Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani. |
Na Walter Mguluchuma, Katavi.
Jeshi la Polisi limefanikiwa kuimalisha ulinzi katika Ziwa Tangamyika hali iliyopelekea kupunguza kwa matukio ya unyang’anyi wa kutumia nguvu uliokuwa ukifanywa na raia wa kutoka katika nchi za jirani na kupelekea sasa ukanda wa ziwa Tanganyika kuwa salama.
Hayo yamesemwa na Naibu Kamishina wa Polisi kutoka makao makuu ya jeshi ambae mkuu wa operesheni maalimu za jeshi la Polisi nchini, Kayo Msekela wakati wa kikao cha wadau wa ukanda wa ziwa Tanganyika kilichowashirikisha pia wakuu wa jeshi la polisi wa Mikoa ya Katavi .Rukwa na Kigoma kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi .Amesema lengo la kufanyika kwa kikao
hicho ni kuishirikisha jamii katika mapambano dhidi ya
uhalifu na wahalifu katika ziwa hilo kwani hapo awali
kulikuwa na mlipuko mkubwa katika ziwa Tanganyika wa
uhalifu .
Amebainisha kuwa ziwa hilo ni tunu kubwa kwa nchi ya Tanzania ambalo linapakana pia na nchi za Burundi , Kongo na Zambia ambao wote tunahaki ya kulitumia kwa kuzingatia mipaka.
Naibu Kamishina Msekela amesema uhalifu ambao ulikuwa umeibuka katika ziwa hilo ulikuwa wa kutumia silaha upolaji wa injini za boti ,samaki na vifaa vinavyotumika kwenye uvuvi baada ya uhalifu huo jeshi la polisi kwa kutumia wadau wanao tumia ziwa hilo kwa shughuli muda wao waliona waanze kukutana na kujadili namna ya kutatua changamoto hiyo .Na tangu wameanza
kufanya vikao hivyo toka mwaka 2022
ni matukio matatu tuu ambayo yametokea kwa kipindi cha
miezi sita ambayo yametokea kwenye ziwa hilo ambapo kwa mkoa wa
Rukwa lipo tukio moja na Mkoa wa Kigoma mawili ya unyang/anyi
wa kutumia nguvu na wahalifu wanaendelea kutafutwa kwani taarifa
wazozipata wahalifu wanatoka Nchi ya Kongo .
Amewahakikishia Watanzania kuwa nchi hii ipo
salama kwenye ukanda wote wa ziwa kwenye Mikoa hiyo
mitatu hivyo wananchi waendelee kufanya shughuli zao
zinazowaingizia kipato alali ila pindi wanapoona kunaviashiria
vya uhalifu watowe taarifa mapema .
Bahati mbaya wahalifu hao wanapofanya uhalifu huwa wanakimbilia kwemye Nchi zao hata hivyo kuna vikao vya ujirani mwema baina ya wakuu wa polisi wa Mikoa hiyo na ukanda wa nchi wanazopakana na kuweza kubadilishana taarifa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amesema vikao hivyo wamekuwa wakivifanya kwa ajiri ya kuimalisha ulinzi na usalama katika Ziwa Tanganyika .Amesema vikao hivyo ni
endelevu kwa ajiri ya kudhibiti uhalifu katika ziwa hilo
kwani wavuvi walikuwa wakipata shida sana ya kupolwa mali zao
wanapokuwa wamekwenda kuvua na kukutana na watu wa nchi nyingine .
Amefafanua kuwa toka wameanza utaratibu
huu matukio yamepungua sana si kama ilivyokuwa hapo awali
kulivyikuwa na matukio makubwa na wanashirikiana kufanya ulinzi na
nchi zinazopakana na ziwa hilo .
Nae mdau wa kikao hicho Diwani wa Kata ya Karema Michael Kapata alisema wahalifu wanaokuwa wamepatikana kwenye ziwa Tanganyika ni vema wakatungiwa sheria kali zaidi.
TANGAZO LA SHULE YA AWALI NA MSINGI YUMA MTAA WA MISUKUMILO MANISPAA YA MPANDA MKOA WA KATAVI.
Wasiliana kwa namba ya simu. 0682 807 755 au 0750 422 103