Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph [Kushoto] akipata maelezo akiwa kwenye banda la Chama Kikuu cha Ushirika Latcu Mkoa wa Katavi kwenye Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi. |
Na Paul Mathias-Katavi
Chama kikuu cha ushirika Latcu
katika mkoa wa Katavi kimeobwa kuendelea kuwasimamia wa kulima wa zao la
Tumbaku kupanda miti ya kutosha kwenye vyama vyao vya msingi kama sheria
inavyosema ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akitoa neno kwenye Banda la Chama Kikuu cha ushirika Latcu kwenye maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi
Chama kikuu cha ushirika Latcu katika mkoa wa Katavi kimeobwa kuendelea kuwasimamia wa kulima wa zao la Tumbaku kupanda miti ya kutosha kwenye vyama vyao vya msingi kama sheria inavyosema ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati
akikagagua Banda la Chama kikuu cha usahirika Latcu katika maonesho ya wiki ya
Mwanakatavi kwenye viwanja vya CCM Azimio Mpanda Mjini.
Amesema kuwa zao la Tumbaku
nimiongoni mwa zao la Biashara ambalo limekuwa likichangia pakubwa pato la
Taifa na kwenye halmashauri za Mkoa wa Katavi na kuwaomba vyama vya msingi kupitia chama kikuu cha ushirika
Latcu Mkoa wa Katavi kuhakikisha Miti inapadwa kwa wakulima wa zao hilo.
‘’Hii miti lazima ipandwe na muikague miti imepandwa wapi kama ekari moja imkulima anatakiwa kupanda miti 300 akiwa na ekari kumi anatakiwa kupanda miti 3000 sasa hili lazima mjilizishe hii miti ipo?-Jamila
Jamila ameeleza kuwa kutokana na
zao la tumbaku kwenda sambamba na Matumizi ya kuni wakati wa ukaushaji wake
lazima upandaji wa miti uwe zoezi endelevu kwa wakulima wa vyama vya msingi ili
kuhakikisha mazingira yanatunzwa.
Katika hatua nyingine ameipongeza
serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kuanza kutekeleza mpango wa kutengeneza Bani
rafiki kwa mazingira ya kukaushia tumbaku
ambayo hutumia kuni kiasi na kuokoa matumizi makubwa ya kuni.
‘’Mabani haya ya kisasa
mmetonyesha hapa nivyema sasa kwenda kuwa simamia wakulima hawa kutumia mabani
haya rafiki kwa mazingira kwa usitawi wa misitu yetu’’-Jamila
Amefafanua kuwa Mazao ya Tumbaku,Pamba, na mazao mengine yanayolimwa kwa kuzingatia kanuni taratibu zake lazima vyama vya ushirika vielimishwe vya kutosha kuhusu sheria ya mazao hayo ili kuwa na usimamizi thabiti.
Kwa upande wake Ramadhan Majaliwa
Bwana aakitoa maelezo kwa Mkuu huyo wa Wilaya katika Banda hilo La chama kikuu
cha ushirika Latcu kwenye maonesho hayo amesema kuwa chama hicho kitaendelea
kuwasimamia wakulima wa zao la Tumbaku na mazao mengine ili kufikia lengo la
uzalishaji.
Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi hufanyika kila mwaka ifikapo Mwezi wa Oktoba ya Kila mwaka kwa Mkoa wa Katavi kwa wakulima na wadau mbalimbali kuonyesha bidhaa zao.