Na Walter Mguluchuma, Katavi
Wananchi wa Mkoa wa Katavi pamoja na Wandishi wa Habari na wanautamaduni wametakiwa kuibua urithi wa utamaduni usioshikika ulioko katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi ili kukuza fursa za uchumi na kuvutia wawekezaji.
Wito huu umetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Afisa utamaduni wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bakari Hamza wakati aliopokuwa akifunga mafunzo ya siku mbili ya Wandishi wa Habari yakuwajengea uwezo wa kutangaza fursa za urithi wa utamaduni usioshikika kwenye Mkoa wa Katavi kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na shirika la Tanzania Media for Community Development kwa ufadhili wa mradi wa UNESCO.
Amewataka washiriki wa mafunzo hayo wayatumie vizuri ili kuhakikisha jamii na kundi la vijana na wasichana kuacha dhana ya kutegemea ajira zinazotolewa na Serikali .
amewaomba watumie vitu vya asili ambavyo vinapatikana katika Mkoa wa Katavi ambavyo hadi sasa jamii ya wananchi wa Mkoa wa Katavi hawavitumii vizuri ipasavyo .
Awali akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Leah Gawaza amewahimiza wandishi wa Habari kutangaza kwa nguvu zote urithi wa utamaduni usioshikika .
Carol Steven Afisa utamaduni na Vijana Mkoa wa Katavi amewahimiza wandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi kutumia nafasi yao kuchangiza kutangaza urithi wa utamaduni wa urithi usioshikika.
Mafunzo hayo yamewashirikisha wasanii wa kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.