Na Paul Mathias-Mpanda
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi ameishukuru serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kuleta fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 2.9 kwaajili ya kuwalipa fidia wananchi 568 wa Kata za Shanwe na Misunkumilo kupisha mradi wa maji wa miji 28 katika manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi ameishukuru serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kuleta fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 2.9 kwaajili ya kuwalipa fidia wananchi 568 wa Kata za Shanwe na Misunkumilo kupisha mradi wa maji wa miji 28 katika manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Kapufi ametoa pongezi hizo wakati
wa hafla ya kukabidhi hundi kwa wananchi iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa
Katavi,kapufi amesema kuwa miongoni mwa jambo ambalo lilikuwa changamoto kwa
wananchi hao ni kutolipwa fidia kwa wanananchi hao.
‘’Jambo hili lilikuwa mfupa mgumu
sana bwana Matyamula hapo na timu yake ilikuwa mkiwa kwenye mkutano wowote
yaani atafata mkutano popote na hoja yake ni kuhusu fidia kwa wananchi wa bwawa
la milala’’-Kapufi
Amempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuleta fedha za fidia kwa wananchi hao ili mradi wa maji uendelee kutekelezwa ili kuwanufaisha wananchi wa manispaa ya Mpanda.
‘’Furaha hii tuipeleke kwa Rais
wetu Dk samia Suluhu Hassan fedha iliyoletwa ni zaidi ya Bilioni 2 ukiacha
mradi mzima ambao unathamani ya Bilioni 22 .8 mradi huu niwa kimkakati lakini
bila fidia kwa wananchi ingekuwa changamoto kutekelezeka kwake’’-Kapufi.
Ameeleza kuwa kilichofanywa na
serikali kwa kuwalipa fidia wananchi hao ni haki yao ya Msingi ambayo wananchi
hao walikuwa wanaisubiria kwa hamu kubwa.
Katika hatua nyingine ameiomba
serikali kuendelea na mchakato wa kuwalipa fidia wananchi waliopisha mradi wa
ujenzi wa barabara ya Mpanda stalike kwakuwa wanaanchi hao wamekuwa wakisubiria
fidia yao kwa muda mrefu sasa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Mwanamvua Mrindoko ameishukuru serikali kwa kuleta fedha hiyo kwaajili
ya malipo ya fidia hiyo kwa wananchi kwakuwa wananchi hao walikuwa na hamu ya
kuona malipo yao yanalipwa kwa wakati.Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumnza na wananchi wa Kata ya shanwe na Misunkumilo kwenye hafla ya kukabidhi hundi ya malipo kwaajili ya kupisha mradi wa maji
Mrindoko amewahakikishia
wanananchi hao zoezi la Malipo litakamilika ndani ya wiki mbili ili wanananchi
wakaanze kuandaa makazi mapya baada ya malipo hayo kufanyika.
Amewaomba wananchi watakao lipwa fidia hiyo kuondoka ndani ya siku Tisini baada ya malipo kufanyika kama walivyokubaliana .
Mradi wa Maji wa Miji 28
unatekelezwa katika Manispaa ya Mpanda kwa Gharama ya shilingi Bilioni 22.8
mradi ambao utagemea chanzo cha Bwawa la milala kama chanzo kikuu cha
upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa Manispaa ya Mpanda.