Na Walter Mguluchuma
Taasisi ya Kuzuia ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imewataka Wananchi katika kuelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu wa 2025 na baada ya uchaguzi wanapaswa kubadilika kutoka kuiona Rushwa kama jambo la kawaida na waanze kuiona Rushwa kama janga lililovamia na tayari lipo kwenye jamii yetu.
Taasisi ya Kuzuia ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imewataka Wananchi katika kuelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu wa 2025 na baada ya uchaguzi wanapaswa kubadilika kutoka kuiona Rushwa kama jambo la kawaida na waanze kuiona Rushwa kama janga lililovamia na tayari lipo kwenye jamii yetu.
Wito huo kwa wananchi umetolewa na Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Stuart Kiondo
wakati wa kikao kazi kilichoandaliwa na Taasisi hiyo kwaajiri
ya kuwajengea uwezo viongozi wa
Asasi zisizo za
Kiserikali Boda boda ,wasafirishaji na wazee maarufu juu ya madhara ya Rushwa wakati wa uchaguzi
na baada ya uchaguzi
Kiondo amesema kikao hicho
ni sehemu ya Takukuru
kuwashirikisha wadau mbali mbali
katika kuomgeza nguvu
za kupambana na Rushwa kwani
kundi hilo walilowapatia mafunzo hayo
na wao wana watu hivyo
watasaidia kuongeza nguvu katika
mapambano ya kupambana na Rushwa .
Kama ambavyo inavyo
fahamika mwaka 2024
itafanyika uchaguzi wa Serikali za Mitaa
na mwakani uchaguzi
mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
hivyo kikao hicho kimejadili juu ya namna bora ya kuwaelimisha wananchi madhara ya Rushwa wakati wa uchaguzi.Baadhi ya washiriki wakiwa katika mafunzo hayo kuhusu madhara ya rushwa katika uchaguzi
Kiondo amesema wananchi
wanapaswa kubadilika kutoka kuiona Rushwa kuwa ni jambp la
kawaida na kuwa ni janga ambalo
limekuwa likirudusha nyuma maendeleo ya watu nan chi kwa jumla .
Leonard Minja afisa mchunguzi wa Takukuru Mkoa wa Katavi amesema
sula la mapambano ya rushwa linahitaji ushirikiano kutoka kwa makundi
mbalimbali ya wadau kwakuwa makundi hayo yanawatu yanao wahudumia.
Leonard Minja afisa mchunguzi Takukuru akitoa elimu kwa makundi hayo
Katibu wa soko la Mpanda
Hotel Haji Mponda amesema Takukuru wanafanya kazi kubwa
sana kwani hata wakifa
leo watakwenda mbinguni kwa jinsi
wanavyotekeleza vizuri majukumu yao ya kazi.
Kwa upnde wake George Kasambwe Katibu wa Taasisi ya Tosovic
amesema takukuru katika kukabiliana na tatizo la rushwa katika kipindi hiki cha
uchaguzi ni muda muafaka sasa kuongeza ushirikiano na azaki ili kukomesha
rushwa.
Kikao kazi hicho kilichoitishwa na takukuru mkoa wa Katavi nimwendelezo wa elimu ya kupinga rushwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi na imeshatolewa kwa makundi mbalimbali ikiwemo waandishi wa Habari,Viomgozi wa dini,viogozi wa kimila na viogozi wa vyama vya siasa pamoja na azaki bajaji na bodaboda