Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akiwahutubia wadau wa Sekta ya Madini Wilaya ya Mpanda kwenye kikao hicho. |
Na Walter Mguluchuma-Mpanda
Serikali ya Wilaya ya Mpanda katika Mkoa wa Katavi imesema kuwa inatambua kazi kubwa inayofanywa
na wadau sekta ya madini
hasa wachimbaji wadogo, wakati
na wakubwa katika kukuza uchumi wa Mkoa
na wa Nchi kwa ujumla na kwa mwananchi mmoja mmoja.
Wadau wa Sekta ya Madini Wilaya ya Mpanda wakiwa kwenye kikao hicho cha wadau wa sekta ya Madini Wilaya ya Mpanda. |
Serikali ya Wilaya ya Mpanda katika Mkoa wa Katavi imesema kuwa inatambua kazi kubwa inayofanywa na wadau sekta ya madini hasa wachimbaji wadogo, wakati na wakubwa katika kukuza uchumi wa Mkoa na wa Nchi kwa ujumla na kwa mwananchi mmoja mmoja.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph
wakati wa kikao cha Jukwaa la wadau wa madini Wilaya ya Mpanda kilichofanyika katika ukumbi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mpanda social Hall .
Amesema wanawapongeza wachimbaji
wote wadogo ,wakati na wakubwa
walioko katika Wilaya ya Mpanda kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuinua uchumi wa wananchi wa Mkoa wa Katavi na kuwapatia ajira wananchi walioko kwenye maeneo ya uchimbaji.
Haidary Sumry Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda akielezea mchango wa sekta ya madini kwa ukuaji wa Manispaa ya Mpanda. |
Amesema
kwa mwaka 2024/2025 ofisi ya madini katika Mkoa wa Katavi walipangiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 7 lakini hadi sasa wameisha vuka lengo kwa kukusanya 7.2 ambazo ni sawa na asilimia 103 mapato
hayo ya madini mengi yametoka katika Wilaya ya Mpanda .
DC Jamila amemshukru Rais
Dkt Samia Suluhu Hassan kwa muhusiano yake mazuri
kati ya nchi yetu ya
Tanzania na Nchi nyingine
Duniani hali ambayo imepelekea
nchi yetu ya Tanzania kuonekana kuwa sehemu
salama kwaajiliya uwekezaji kwenye sekta ya Madini.
Amefafanua kuwa sekta ya madini
ni sekta inayokua kwa kasi sana katika
Wilaya ya Mpanda ambayo imekuwa inakuwa
kila siku na imekuwa ikipokea wawekezaji
wengi kutoka nje ya wilaya na nje nchi kwa ajiri ya uwekezaji .
Mwandisi Alex
Mwidunda kutoka kutoka ofisi ya Afisa
madini Mkazi Katavi amesema kuwa
madini ambayo yanapatikana Katavi
yapo ya aina sita ambayo ni Dhahabu
,Shaba , Galena ,Mica (ulanga) madini ya ujenzi na mika .
Mchimbaji mdogo wa madi ya dhahabu George Kalasi ameiomba serikali iona namna ya kuweza kuwasaidia wachimbaji kwa kuwapunguzia baadhi ya kodi za tozo.