![]() |
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya ziwa Tanganyika Imani Kibona akitoa neno kwa wageni walioshriki hafla hiyo. |
Na Walter Mguluchma-Katavi
Askofu
wa Kanisa la KKKT
Dayosisi ya Ziwa Tanganyika Askofu
Iman Kibona wananchi wa Mkoa wa Katavi wadumishe
amani wakati wa kipindi cha sikukuu ya pasaka na baada ya pasaka kwani wanapaswa watambue kuwa amani
ni tunu imetoka kwa Mungu .
![]() |
Wito
huu ameutowa wakati kati wa hafla ya chakula cha jioni
iliyoandaliwa Dayosisi ya
Ziwa Tanganyika Ushirika
wa Nazareth Mpanda
kwa ajiri ya kuchangia ujenzi wa
makazi ya nyumba ya mchungaji wa
ushirika huo na mgeni Rasmi
alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Onosmo Buswelu .
Amesema
amani ni tunu ambayo tumepewa na
Mungu hivyo anawasihi sana waumi na
wasio waumini washerekee sikukuu ya
Pasaka wakiwa wanadumisha amani kwenye
familia zao kwani amani ya kwanza inaanzia kwenye familia .
Amebainisha
kuwa familia ikiwa na amani waumini na wasio waumini wanakuwa na amani na hivyo watakuwa wanadumisha amani kwenye
maeneo wanayoishi .
Askofu
Kibona amewasisitiza wananchi wailinde na kuitunza amani ya nchi yetu kwani
inategemewa kulindwa na watu wenyewe na
ndipo tunapo weza kukaa kama ambavyo tunavyoishi sasa kwenye nchi
nyingine hali sio nzuri na tunapo
ona hivyo tusifurahie bali na wao tuwaombea .
Katika
hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Mwanavua Mrindoko iliyotolewa kwa
niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amesema Serikali ya
Mkoa wa KatavI wanayo nia ya dhati kabisa inayoongozwa
na Rais Dkt Samia
Suluhu Hassan kuwaelekeza viongozi wote wa serikali kufanya kazi
kwa kushirikiana na madhehebu
yote ya dini .
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Katavi amewaomba viogozi wote wa dini wapande miti ya matunda kwenye maeneoyao yao yanayozunguka nyumba zao za ibada na wanayomiliki ili kuweza kupata matunda yatakayosaidia kukabiliana na hali ya udumavu katika Mkoa huu.