TAKUKURU  KATAVI  WAOKOA  ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 29

 

Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Stewart Kiondo

Na Walter Mguluchuma

     Katavi .

Taasisi ya  Kuzuia na  Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi wamefanikiwa kuokoa  kiasi  cha zaidi ya shilingi milioni  29 kufatia kazi  walizofanya   kwa kipindi cha miezi mitatu  za  kuzuia  Rushwa  na uchunguzi .





Hayo yameelezwa na Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Stewart Kiondo wakati alipokuwa akitowa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo  mbele ya wandishi wa Habari ya  kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Oktoba   hadi Desemba 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi .

Amebainisha kuwa Takukuru  Mkoa wa Katavi  katika  kipindi hicho cha miezi mitatu ya utendaji wao wa kazi  wameweza  kuokoa  kiasi cha tsh  29,994 ,982kupitia  kazi za uzuiaji  wa Rushwa  uchunguzi  na kusaidia  kuongezeka kwa mapato  ya Halmashauri .

Amebainisha kuwa  tshs 12,000,000 zimerejeshwa  baada  ya kubainika  nikopo ya  asimilia 10 iliyotolewa  na  Halmashauri ya  Mpimbwe  kwa kikundi cha  wanawake  ilitumika  kwa  matumizi  yasiyokusudiwa  kufatia  ufatiliaji  wa Takukuru  fedha hizo zilirudishwa   na kuwekwa  kwenye  akaunti  ya  Wanawake ,vijana  na  watu wenye ulemavu .

Kiondo   amesema tshs  17,994,982 zimerejeshwa kupitia  hatua za uchunguzi  na mashitaka  baada  ya washitakiwa  katika mashauri mbalimbali   kuingia makubaliano  ya kisheria (plea Bargaining) fedha ambazo zilihusisha  mapato ya ndani  yalikusanywa kupitia mfumo wa POS na aziwekwa Benki kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na   zilikuwa zimetumiwa kwa matumizi yasiyokusudiwa .

 

Kuhusu  malalamiko  kwa kipindi hicho wameweza kupokea jumla ya malalako  32 kati  ya malalamiko hayo   17  yalihusu tuhuma za Rushwa  na yaneandelea na uchunguzi  ambapo malalamiko  15  hayakuhusu tuhuma za Rushwa na walalamikaji  walishauriwa na kuekekezwa sehemu sahihi ya kupeleka .

 

Kiondo amesema  Takukuru Mkoa wa Katavi  wameweza kushinda kesi tatu   walizopeleka Mahakamani  na wamefungua kesi  mpya   mbili  huku kesi 10 zikiwa  zinaendelea  kusukilizwa Mahakamani  zikiwa  zimesikia hatua mbalimbali .

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages