![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph |
Na Walter Mguluchuma, Katavi.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Jamira Yusuph ametowa shukurani za dhati kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Mpanda kwa namna ambavyo Rais ameendelee kuwaletea fedha nyingi kwa ajiri ya utelezaji wa shughuli mbalimbali za Maendeleo.
Jamila ametowa shukurani hizi wakati alipokuwa akiwahutubia wajumbe wa mkutano wa Kamati ya ushauri ya Wilaya ya Mpanda (DCC) kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Amebainisha kuwa hata wajumbe wa kikao hicho watakuwa ni mashahidi kwa fedha nyingi za utekeleza wa shughuli za maendeleo zilizopelekwa katika Wilaya ya Mpanda kwani kwa mwaka huu wa fedha Halmashauri ya Nsimbo wameisha pokea kiasi cha Shilingi bilioni 14 na Manispaa wamepokea bilioni 16 ambazo zimeenda kwenye shughuli za maendeleo na majeti hiyo bado inaendelea.
![]() |
| Mzee Vicent Nkana akichangia mada katika kikao cha DCC |
Amesema kwa mwaka wa fedha ujao wa 2026/2027 bajeti za Halmashauri mbili zilizopo latika Wilaya ya Mpanda zimeongezeka kwa mfano Manispa ya Mpanda Bajeti iliyopita ilikuwa ni bilioni 33.9 lakini bajeti ijayo ni Bilioni 35.2na Nsimbo ilikuwa Bilioni 27.4 bajeti ijayo ni Bilioni 35.7 na pia kwenye Taasisi nyingine za Serikali bajeti imeongezeka.
Dc Jamila ameeleza kuwa kwenye mapato ya ndani pia yameingezeka kwa Halmashauri zote mbili mwaka wa fedha uliopita mapato ya ndani ilikuwa ni Bilioni 6.7 kwa bajeti ijayo mapato ya ndani ni bilioni 7.5 mbali ya bajeti fungiwa ongezeko hilo ni matumaini makubwa kwa wananchi wa Wilaya ya Mpanda kama ilivyo dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea Maendele wananchi .
Mzee maarufu wa Wilaya ya Mpanda Vicenti Nkana amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Mpanda kwa kuwa wamekuwa ni watu wa kwanza kugundua makosa yanapokuwa yametokea na kuyafanyia kazi mapema na kutatua.


