Na Walter Mguluchuma, Katavi.
Kampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku PREMIUM ACTIVE TANZANIA imetowa dawati 300 zenye thamani ya Zaidi ya shilingi Milioni 29 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwenye maeneo yanayolima zao la tumbaku ikiwa ni mchango wa maendeleo ya jamii kwenye maeneo yanayo lima tumbaku kwenye Halmashauri hiyo katika kuunga mkono jitahada za serikali za kuboresha sekta ya elimu hapa Nchini.
Meneja Shughuli wa Kampuni ya Premium ACTIVE Tanzania Nico Roussos amekabidhi mchango huo wa maendeleo kwa jamii mawati 300 kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu
Roussous amebainisha kuwa lengo la kukabidhi dawati hizo 300 ni mchango wa Kampuni ya PREMIUM Active Tanzania ni kwa ajiri ya kusaidia kwa kurudisha faida sehemu ya faida inayopatikana kwa wabia wao wao wakulima wa tumbaku ambao ni wananchi wa wilaya ya Tanganyika.
Amesesema katika kufanikisha zoezi hilo la kurudisha sehemu ya faida inayopatikana kampuni hupokea kipaumbele cha mahitaji kutoka katika sehemu husika kwenye maeneo ya Kata zenye vyama vya ushirika vya msingi vinavyofanya kazi na Kampuni ya premium.
Kwa Mkoa wa Katavi walipokea maombi ya kutengenezwa madawati 753 yenye thamani ya shilingi milioni tshs 77,990,576.22 kati ya madawati hayo Wilaya ya Tanganyika wao wamepewa madawati 300 kwa ajiri ya shule za awali na msingi .
Roussous amefanunua kuwa kwa mwaka 2026 kampuni ya Premium Active inatowa mchango wa maendeleo ya jamii kwa Halmashauri za Wilaya nane hapa nchini ambapo wamechangia madawati kwa shule za msingi na sekondari Pamoja na vifaa vya ujenzi ,michezo mbalimbali ambapo jumla ya thamani yote ikiwa ni Tshs 162,832,737.06
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu wanaipongeza kampuni ya Premium kwa kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuchangia mahitaji katika sekta ya elimu hapa nchini.
Amewaomba wadau wengine wainge mfano wa kampuni hiyo katika kugusa mahitaji ya Watanzania na wameisha jipanga kuhakikisha kila dawati linafika haraka sana kwenye eneo usika siku hiyo hiyo.
Buswelu amesema kwa namna nyingine wanafunzi watakao yakalia madawati hayo wazazi wao ni wakulima wa tumbaku hivyo watafahamu kuwa kampuni ya Premium imewachangia madawati wataendelea kukumbuka kuwa kilimo cha tumbaku pia kinaleta madawati.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanganyika Shabani Juma amesema madawati hayo yatawasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa madawati wao pia kama Halmashauri wanazo pia juhudi za utengenezaji wa madawati na wameisha wameisha towa tenda ya kutengeneza madawati 3,600


