NSSF KATAVI KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA

 




Na Abdi Lunyamila.

Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF limewataka Wananchi Wanachama kuendelea kutoa taarifa zao za mfuko pale wanapo ona changamoto au kutokuwepo kwa michango yao ili kuwezesha mchakato wa uboreshaji huduma kwa Wateja.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Katavi Ndg.Jacob Sule Wakati wa maadhimisho ya siku ya kutoa Huduma kwa wateja yaliyofanyika tarehe 05 mwezi wa 10 2026 Mpanda mjini katika Ofisi za NSSF Mkoa wa Katavi.

Sule amebainisha kuwa hatua hiyo ni muhimu ili kuhakikisha taarifa zote zinakuwa sahihi na kulinda haki ya kupata mafao ya Wanachama kwa wakati bila kusuasua tofauti na  ilivyo kuwa miaka ya nyuma ambapo baadhi ya Wanachama wamekuwa wakifuatilia mafao yao kwa muda mrefu sana.


Aidha ametoa wito kwa mashirika mbalimbali hususani mashirika binafsi kwa mujinu wa sheria kwa kuhakikisha michango ya Wanachama inawasilishwa kila mwezi tena kwa wakati kwa sababu hatua hiyo ni muhimu katika kulinda haki za wafanya kazi na kuhakikisha wanapata stahiki zao wanapo hitaji.

Amesema Nssf bado inatambua ya kwamba kuna maeneo bado yanahitaji maboresho ikiwepo kuongeza uelewa kwa wateja kuhusu haki na wajibu wao na kuhakikisha kuwa michango inawasilishwa kwa wakati “NSSF itaendelea kushuhulikia changamoto hizi kupitia utoaji wa Elimu,ufuatiliaji na uboreshaji wa utoaji wa huduma kwa Wateja na kwa upande wetu Watumishi tutahakikisha tunasimamia uchapa kazi haki na uadilifu ili huduma bora kwa vitendo isiishie kauli mbiu yetu ya maadhimisho haya”. Amesema Sule

Kwa upande wao wanachama wamesema Watoa huduma wa Nssf wanatakiwa kuwa na moyo wa upendo pindi wanapo wahudumia, vilevile kutoa Elimu kwa Umma kitu ambacho kitaleta motisha kwa Wananchi wengine ambao bado hawajaiunga na hatimaye kujiunga.

 

 

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages