AJINYONGA KWA WAYA MWEUSI NA KUACHA UJUMBE MZITO..

Na Neema Hussein KTPC,Mpanda.

Kijana aliyefahamika kwa jina la Twaibu Omary (22) amefariki dunia baada ya kukutwa bafuni akiwa amejinyonga kwa kutumia waya mweuzi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,Abdi Isango amesema tukio hilo limetokea katika Kata ya Nsemlwa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Amesema siku moja kabla ya kifo chake Marehemu alitofautiana kauli na Mama yake mzazi kuhusu mabishano ya kisiasa ambapo marehemu alikuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mama yake ni Chama  Cha Mapinduzi(CCM)

Isango amesema kuwa kutokana na mabishano hao Mama yake aliksasilika na kuamua kumpiga makofi mtoto wake.Hivyo mtoto alikataa kula chakula alichopika mama yake na kuamua kuondoka na kurudi usiku nyumbani.

Amesema siku ya tukio Mama aliondoka asubuhi na mapema kuelekea kazini ndipo kijana huyo aliipochukua maamuzi ya kuchukua waya na kuingia bafuni kujinyonga huku akiwa ameacha ujumbe ambao aliubandika kwenye ukuta wa bafu hilo uliosomeka '' in the life there is two options to live or  to leave  and i choice to leave''

Mama mzazi wa marehemu amesema mtoto wake alikuwa anapenda kusoma lakini alishindwa kumtimizia ndoto zake kutokana na kipato chake kuwa kidogo.

''Twaibu alipenda sana kusoma ila nimeshindwa kumsomesha kwa maana pesa nilikuwa nategemea kulipwa ba Kampuni ya Riga Mining ambayo naidai milioni tisi na laki nne na sitini elfu ili yeye asome,ila nimefuatilia kesi hiyo ya madai bila mafanikio yoyote hadi sasa'' amesema mama huyo. 

Amesema baada ya mwanaye kuona anafatilia kesi bila mafanikio alimwambia hawezi kuendelea na kumuona anateseka bila mafanikio hapo ndipo alipomuuliza mama yake kuwa CCM imemsaidiaje ili kupata fedha zake za madai?,ndipo mabishano yalizidi  ya vyama vya siasa huku marehemu akimtaka mama yake kuhama chama hicho.

Kwa upande wao baadhi ya majirani wamesema kuwa marehemu alikuwa ni mtu muhimu kwenye jamii kwani aalipenda kusoma japo alifanya kazi ya bodaboda  kutokana na kukosa msaada wa yeye kupata elimu.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages