WANANCHI WA MTAA WA NSEMLWA WAKERWA NA UBOVU WA BARABARA.

 

Barabara ya Nsemlwa Mkumbo ikiwa katika mwonekano mbovu zaidi huku wananchi wakipata usumbufu wa kupita.

Na Alex Ngeleza KTPC,Mpanda.

Baadhi wa Wananchi na Wakazi wa Mtaa wa Nsemlwa wameelezea hisia zao baada ya kukerwa na ubovu wa miundombinu ya barabara inayotoka katikati ya mjini kuelekea mtaa huo wa Nsemlwa Mkumbo.

Wananchi hao ambao binafsi hawakutaka majina yao kutajwa ndani ya blog hii,Wameeleza kuwa serikali ya Mkoa ni kama haijali kwa kile kinachoendelea katika barabara yao kwani kwa sasa ni mbovu zaidi.

Wasema kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu sana cha Manispaa kutokana na idadi ya wingi wa watu wanaoishi katika mtaa huo,Huku wakisisitiza kuwa ubovu huo wa barabara unautia aibu Manispaa kama makao makuu ya Mkoa kwani kiuharisia bado ni miongoni mwa barabara ziko karibu sana na mjini.



Hivyo wameiomba Tarura Manispaa ya Mpanda kuwa inaondoa kero hiyo ambayo kwa muda mrefu wamekuwa wakiteseka licha ya kuahidiwa kila mara kuwa barabara hiyo itatengenezwa.





Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages