Na George Mwigulu KTPC,Tanganyika.
Kupitia Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Tanganyika Mkoa wa
Katavi,Vijana wamenufaika na mafunzo ya mlipa kodi na ushuru mbalimbali yaliyotolewa na Mamlaka
ya Mapato Tanzania(TRA) mkoani humo ili kuwajengea uzalendo kwa taifa na
kuwajibika kulipa kodi.
Mafunzo hayo
yametolewa na TRA wakati wa kuelekea maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa chama
cha Mapinduzi (CCM),ambapo kabla ya kilele kitakachofanyika 5,Feb mwaka huu kumefanyika semina maalumu ya
kiitikadi kwa umoja wa vijana hao
wilayani Tanganyika.
Emmanuel
Msava,Afsa huduma na elimu kwa walipa kodi wa mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa
Katavi akitoa mafunzo hayo jana kwenye semina ya kiitikadi katika ukumbi wa
shule ya sekondari Kakoso ameeleza kuwa walipa kodi wanapaswa kupewa elimu pamoja na mamlaka
hiyo kuwa na wajibu wa kuhakikisha walipa kodi wanapata huduma kwa kiwango cha juu
ambacho serikali imepanga kukitoa.
Afsa huduma huyo amefafanua kuwa licha ya mlipakodi anapaswa kusajiliwa na kupewa TIN namba ambayo inamwezesha kupitia biashara yake anayoifanya kulipa kodi pia anapaswa kulipa kodi kikamilifu kinyume na baadhi ya wafanya biashara kuona pekee umuhimu wa kuwa na TIN huku wakikwepa kulipa kodi.
‘’ lengo la
kusajiliwa na kupewa TIN namba ni kuwa mfanyabiashara unapaswa kulipa kodi na
kama mwananchi unapaswa kuhakikisha kuwa kodi hiyo inaingia serikalini kwa
kuomba listi pale unaponunua bidhaa’’ alisema Msava.
Akiwafundisha
nani anapaswa kulipa kodi na umuhimu wa
kulipa kodi alisema kuwa kodi inatokana
na vyanzo vitatu ambavyo ni ajira,biashara pamoja na uwekezaji ambapo aina ya
kodi hii inatozwa kwa mamlaka ya sheria ya kodi ya mapato.
Umuhimu wake
ni kusaidia uchumi wa taifa kupanda na kusaidia katika kuendesha shughuli
nyingi za kitaifa.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi David Mussolin amesema mafunzo
hayo ya kiitikadi yanatokana na maelekezo waliyopewa kutoka makao makuu ya
chama hicho ili kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo wa kiitikadi na imani ya
chama pamoja na mambo mengine.
Mussolin amesema kuwa mafunzo hayo ya kiitikadi na
imani yatawawezesha vijana kuwa na juhudi za kuelewa,kuieleza ,kuitetea na kuitekeleza itikadi ya CCM.
Vijana wa\ Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika hali ya utulivu wakisikiliza kwa umakini mafunzo maalumu ya kiitikadi na imani kwa chama chao. |
Awe kijana ambaye siku zote yuko mstari wa mbele katika utekelezaji wa mambo ya uanachana ,sera,miongozo ,kanuni ya UVCCM na katiba ya CCM.
Aidha
kuwawezesha vijana kuwa wanaoheshimu watu mwenye tabia nzuri ,muaminifu
,muadilifu mwenye kauli na vitendo vizuri mbele ya jamii huku asiyetoa wala
kupokea rushwa au mapato mengine ya kificho.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wila\ya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi,Ndg David Mussolin akizungumza na vijana kuhusu umuhimu wa kuwa wazalendo katika kulitumikia taifa. |
Secilia
Samweli Mkazi wa kata ya Isengule
wilayani humo ambaye ni mshiriki wa mafunzo hayo ya kiitikadi ameshukuru chama kwa kuandaa mafunzo hayo
kwani moja ya mambo alikuwa hana ufahamu nayo ni kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.
Hivyo
amebainisha kuwa kwa sasa amefahamu kwa upana zaidi namna ambavyo inampasa kuwa
balozi wa TRA katika kuelimisha watu umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kudai
lisiti baada ya kununua bidhaa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Isengule Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi,Ms Secilia Samweli. |
Vilevile
amesema kuwa mafunzo ya mada mbalimbali ya kiitikadi na imani kwa chama chake
yamemwongezea nguvu ya kuwezo wa kukitetea
na kukielezea chama kwa ufasaha zaidi.