Baadhi ya Matrekta yaliyopo Mkoa wa Katavi ambapo yanatumika kwa sasa katika kilimo. |
Serikali ya Mkoa wa Katavi imekusudia kuongeza uzalishaji kwa wingi wa mazao mbalimbali ya nafaka ili kufikia malengo ya kuzalisha zaidi ya tani milionii tatu.
Ambapo uzalishaji uliopo sasa ni kutoka tani laki tano za mahindi,tani laki nne za mbunga hadi kufikia yani milioni tatu kwa msimu wa kilimo 2020/21 ili kufikia lengo la kuhudumia chakula nchi za SADEC ikiwa ni baada ya wananchi kuhimizwa kuanza kutumia kilimo cha kutumia zana za kisasa na kuachana na kilimo cha jembe la mkono.
Tangu kuanzishwa kwa Mkoa wa Katavi mwaka 2006 wakulima wa mazao mbalimbali wamekuwa wakitumia zana za jembe la mkono licha ya mkoa huo kuwa na fursa za uzalishaji wa kilimo na kufikia kushika nafasi ya nne kitaifa kwa msimu wa mwaka 2019.
Kampuni ya uuzaji wa zana za kilimo Lonagro Tanzania LTD ambayo wanajihusisha na uuzaji wa matrekta ya kilimo wamefika mkoani Katavi ili kuwarahisishia wakulima kupata zana za kilimo kwa urahisi zaidi kwa kuwa karibu zaidi tofauti na ilivyokuwa hapo awali na Meneja wa Kampuni hiyo Tawi la Mpanda Mjini Peter Likecha ameeleza mafanikio makubwa ambayo wakulima watayapata kwa kutumia zana hizo.
Meneja wa kampuni ya Lonagro Mkoa wa Katavi,Peter Likecha akitoa lengo la kampuni hiyo la kuhamasisha wakulima kuachana na kilimo cha jembe la mkono |
Wakuu wa wilaya ya Mlele na Tanganyika Mkoa wa Katavi wameeleza kuwa mkoa unategemea sana mapato yatokanayo na sekta ya kilimo na zana hizo za kisasa zitaleta mapinduzi ya kilimo.
Baadhi ya wadau wa kilimo Salum Sumury aliyekuwa mmiliki wa Mabasi ya Sumury wameeleza kuwa sekta ya kilimo ni moja ya nguzo muhimu kwa kuipeleka nchi kwenye mapunzi ya viwanda,Hivyo kama serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa kilimo wataweza kuimarisha sekta hiyo kuanzia katika kubadili aina ya mfumo wa kilimo nchini na kuwa wa kisasa wa kutumia matrekta.
Sumury alifafanua kuwa kilimo cha kutumia matrekta ndiyo kimebeba mwarobaini wa kuondokana na uzalishaji wa mazao ya kilimo yaliyo duni.