Jidith Abdallah Afisa ntumishi Mkuu kutoka Ofisi ya Rais manejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora [Kulia]akimsikiliza mmoja wa walimu waliofika kuwasilisha kero zao za kiutumishi. |
Ofisi ya Rais management na utumishi wa umma na utawala bora
imepiga kambi katika mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na chama cha walimu [CWT] kwa
lengo kusikiliza changamoto za walimu na kuzifanyia uchambuzi na kuzitatua
nanyingine kuziwasilishia mapendekezo ili kupata utatuzi wake.
Baadhi ya maafisa kutoka ofisi ya Rais menejimenti na utumishi wa umma na utawala bora wakimpa ufafanuzi moya ya nwalimu alifika kutatuliwa changamoto yake ya kiutumishi. |
Hayo yamebainishwa na Judith Abdallah Afisa utumishi Mkuu kutoka
ofisi ya Rais management na utumishi wa umma na utawala bora wakati alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa milkutano wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Mpanda.
Ameeleza kuwa wamefika mkoa wa Katavi kwa lengo la kusikiliza kero
za walimu kuzipatia utatuzi na zingine kuziwasilisha kwaajili ya kupatiwa
majawabu ikiwemo masuala ya kimuundo malimbikizo na kwawale waliochelewa
kupandishwa madaraja yao utumishi.na wale waliojiendeleza na hawajafanyiwa mabadiliko
ya kimuundo.
Amesema kuwa ofisi hiyo imekasimishwa majukumu ya kusimamia utumishi wa umma kwa kuzingatia sera sheria kanuni na miongozo mbalimbali ili kuhakikisha watumishi wa umma wanaweza kutatuliwa matatizo yao lakinin pia wanakuwa wakitekeleza majukumu yao katika mazingira mazuri ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi ili kusaidia nchi kutimiza malengo yake.
Mwalimu Peter Maganga wa shule ya Msingi Mtisi Halmashauri ya
Nsimbo Mkoa wa Katavi amesema amefurahishwa na zoezi hilo lililowafikia walimu
wa Mkoa wa Katavi na amekishukuru cha cha walimu [CWT]kinafanya kazi ya kubwa
ya kuwapigania walimu.
Maganga amewasisitiza walimu wa Mkoa wa Katavi waendelee
kukiungamkono chama chao cha CWT kwa kufanya kazi ya kuwaleta viongozi kuja
kusikiliza kero mbalimbali za walimu kwenye Mkoa wa Katavi zinazohusiana
upandishwaji wa madaraja na mapunjo ya mishahara na mambo mengine ya kiutumishi
‘’Mimi ni mmoja ya wahanga nilikuwa nahitaji daraja la mseleleko nimefika kwa maafisa kutoka wizarani wamenisikiliza wameangalia taarifa zangu katika mfumo wamehakiki ninasifa ya kupanda daraja japo sijpanda daraja langu moja wamelichukua na wanaenda kulifanyia kazi’’-Maganga
Mwalimu Peter Maganga wa shule ya Msingi Mtisi Halmashauri ya Nsimbo akishukuru kero yake kwa kutatuliwa. |
Amefafanua kuwa amefurahishwa kwa kuzikuta taarifa zake sahihi kwenye mfumo huku akishukuru CWT kwa kutunza taarifa sahihi ambazo zimesaidia maafisa kutoka ofisi ya Rais Manegementi ya utumishi wa umma na utawala bora kubaini changamoto zao walimu.
Kwa upande wake Mwalimu Peter chitokalomo kutoka Halmashauri ya
Uyui Mkoa wa Tabora amesema kuwa amefika Mkoa wa Katavi kwaajili ya kutatuliwa
tatizo la kutopandishwa daraja na baada ya kupata taarifa ya uwepo wa maafisa
kutoka utumishi wa umma na utawala bora na tatizo lake limeweza kutatuliwa na
maafisa hao na amerejea Tabora.
Aameishukuru serikali kwa kuanzisha huduma hiyo ambapo watumishi
wanapata fursa ya kuhudumiwa moja kwa moja mahali walipo amekishukuru chama cha
walimu [CWT] kwa namna ambavyo wamehusika katika kushirikiana na serikali kutatua
changamoto zao walimu.
Baraka kitenya Kaimu Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Katavi amesema kuwa anaishukuru serikali kwa kuja na mpango huo ambao umekuwa na tija kwa walimu kusikilizwa kero zao kwa wakati zinazo husu Madaraja na mambo ya mapunjo ya mishahara.
Kitenya amebainisha kuwa jambo hilo limewagusa sana walimu na wametambua serikali ipo kazini na iwajali walimu kwa vitendo na wanaamini baada ya zoezi hilo mkoa wa Katavi utakuwa umepunguza changamoto zinazo wakabili walimu.