Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera akiwa kwenye moja ya trekta akifanya majaribu ya kuiwasha |
Na George Mwigulu KTPC,Katavi.
KILIMO ni moja ya sekta muhimu kwa uchumi hasa kwa mataifa mengi ya Afrika yanayotegemea uzalishaji bora wa mazao ili kuinua uchumi wa wananchi wake.
Serikali ya Tazania kwa kutambua umuhimu wa kilimo imehakikisha
wakulima wanajikwamua kwenye mdororo wa uchumi kwa kufungua milango kwa taasisi
na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali (NGO) kwa kushirikiana na
wataalamu wa serikali watoe elimu ya kutosha kwa wakulima ili waachane na
kilimo cha mazoea na kujikita katika kilim biashara chenye tija.
Kwa muktadha huo Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) kwa kushirikiana na
Shirika la Maendeleo (ADP-MBOZI) kwa ufadhili wa Shirika la Mapinduzi ya
Kijani Afrika(AGRA) wanatekeleza mradi wa TIJA-TANZANIA katika
halmashauri ya Nsimbo,Mlele,Mpimbwe,Tanganyika na Manispaa ya Mpanda Mkoani
Katavi ambapo matokeo makubwa yameonekana.
Shirika la Mapendeleo ADP Mbozi linashughulikia uzalishaji na kuimarisha vikundi vya wakulima huku Baraza la Kilimo Tanzania(ACT)likijikita katika ugumbuzi wa changamoto za masoko na udhibiti wa upotevu wa mazao.
Ofsa Mradi wa Tija-Tazania Edward Mwakagile amesema kuwa shirikisho
hilo limefanikiwa kupata ufumbuzi wa kimazingira ya Afrika ili kuongeza
uzalishaji endelevu wa mazao ya wakulima na kuwaunganisha na masoko ya mazao
yao.
Hivyo mradi Tija Tanzania ,mkoa wa Katavi umeshiriki kikamilifu
kumpa kipaombele mkulima hasa mdogo aachane na kilimo cha kujikimu hali
iliyochochea kasi ya uzalishaji na mavuno bora ambapo yameuwezesha mkoa
huo kushika nafasi ya nne kitaifa kwa uzalishaji wa chakula cha ziada.
Anasema kuwa mradi wa Tija Tazania umeanzishwa mwaka 2017 na
ukitarajiwa kumalizika ifikapo octoba 2020 ukiwa na lengo la kuongeza
uzalishaji wenye tija kwa wakulima wadogo wadogo ili kuwa
na uhakika wa chakula na kuongeza kipato kwa wakulima.
Kuhakikisha uzalishaji wa chakula unaongezeka hususani mahidi,maharage na
mpunga mradi umejikita katika kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa
pembejeo.
"...mradi unahamasisha wanawake pamoja na vijana washiriki kwenye masuala
ya uzalishaji na kumiliki vyanzo vya mapato na vya kiuchumi kwenye sekta ya
kilimo ikiwa na kuziona fursa zilizopo na kuzitumiakuongeza kipato cha
familia",Alisema afsa huyo.
Kufanya kazi na vikundi vya wanawake na vijana kumewasaidia kuzitumia
fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo kuongeza mapato ambapo wamefanikiwa
kupata zana za kilimo za kisasa kama vile majenereta za umwagiliaji,mashine za
kukatia mpunga ili kurahisisha shughuri za uvunaji wa mbunga.
Aidha vikundi vingine vimefanikiwa kupatiwa mashine za kupula mpunga kama
nyenzo muhimu kwenye kilimo ambapo teknolojia zote hizo zimesaidia wakulima na
hatimaye wameweza sasa kujihushughurisha na kilimo hata kwenye mazingira ya
kiangazi.
Mwakagile anaweka wazi kuwa baada ya utafiti uliofanywa na ACT ulibaini
Mkoa wa Katavi uzalishaji wake hapo awali ulikuwa chini sana ,kwa upande mahidi
wakulima wadogo wadogo kwa hekali moja walikuwa na uwezo wa kupata gunia tatu
hadi tano ikiwa kwa mpunga kila hekali walikuwa wakivuna gunia tano hadi kumi
na tano pekee.
"...baada ya utafiti ilionekana kwamba changamoto kubwa ni matumizi
duni ya pembejeo na mbegu bora za kisasa ikiwa pamoja na uhaba wa upatikanaji
wa elimu ya kilimo ilikuwa shida hasa ukizingatia maeneo ya mkoa ni makubwa na
watumishi wa serikali walikuwa wachache kuhakikisha wanamfikia kila
mkulima"Alisisitiza Mwakagile.
Kwa kutambua changamoto hizo Mradi wa Tija Tanzania umefanyika
kwa mfumo wa ushirikishwaji pamoja na serikali ngazi ya mkoa hadi ngazi
ya wilaya, ambapo katika ngazi ya wilaya waliteuliwa wasimamizi wa mradi wa
kila wilaya na hao ndio wasimamizi na waratibu wa mradi katika
halmashauri.
Katika kuwawezesha wakulima wametumia mfumo wa wagani kazi vijijini na
vitongoji ambao waliwateua miongoni mwa wakulima na kuwapatia mafunzo ya
msingi ya elimu ya kilimo bora ambapo walitumika kutoa elimu kwa wakulima
wengine kwa ukaribu zaidi.
Mbinu zingine ambazo zimetumika ni kutumia mashamba darasa zaidi ya elfu moja
kwa kugawa mbegu bora ,mfano kwenye mashamba hayo,warsha mbalimbali pamoja na
kutumia sikuu za nane nane kuwapeleka wakulima ambayo yote hiyo ni jitihada za
kuhakikisha wakulima wanapata elimu ya namna ya uzalishaji wa mazao bora.
Anasema " kitendo cha kuwapeleka kwenye maonesho ya nanenane imewasaidia kukutana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye uzalishaji ambao wakulima wengine wanafanya ili nao waje waitumie kwenye mashamba yao".
Hatua ambazo zimechukuliwa baada ya mradi huo kufikia mwishoni amesema Mwagaikile kuwa kama mwaka mitatu wameweza kufanya kazi na wagani kazi zaidi ya 316 na mabwana shamba wa halmashauri pamoja na wasimamizi wa mradi kwa ngazi wilaya na kuwafikia zaidi ya wakulima 36,000.mfumo wenyewe unajitoshereza kujiendeleza.
Willlison Lotti Ofisa mradi wa baraza la kilimo Tanzania amesema kuwa
mradi wa Tija Tazania umewakomboa wakulima kwenye sekta ya
masoko ambapo kwa miaka mingi wemeshindwa kupata.
Lotti amefafanua kuwa halmashauri ya Mlele,Mpanda na Tanganyika kutokana na
hapo awali kutokuwa na mfumo mzuri wa kufanya biashara na usindikaji,Wakulima
wengi hawakuwa kwenye vikundi na kupelekea kuuza mazao yao kiholela.
Kwa sababu ya kuuza mazao kiholela na kuzalisha mazao yasiyonauhitaji sokoni
ilipelekea mazao kuuzwa kwa bei ndogo inayomkandamiza mkulima na kumwacha
masikini.
Moja ya shamba la Mahidi Mkoani Katavi ambapo yanazalishwa kwa wingi. |
Baada ya utekelezaji wa mradi wa Tija Tanzania kuanza kitu ambacho baraza la kilimo Tanzania kupitia mradi huo imefanya ni kuhamasisha wakulima kujiunga kwenye vikundi ili waweze kufikiwa na wanunuzi wa mazao kwa urahisi ikiwa pamoja na kuwa na uwezo wa kukubali au kukataa bei ambayo wanaona haina masirahi kwao.
"...kutokana na mazao kukosa ubora unaotakiwa kwa uchafu uliochanganyikana na mchanga na mawe pamoja na kuchanganya bidhaa wanayotoa shambani na bidhaa nyingine ambazo hazihitajiki kuwepo kwenye zao husika"asema Lotti.
Baraza hilo limehamasisha wakulima 52,000 na kupewa mafunzo na baraza la kilimo ya namna ya kuhifadhi mazao baada ya kuyavuna na kusababisha hivi sasa mazao yanayouzwa kwa wasindikaji kuwa na ubora unaohitajika.
Vilevile kwa kuhamasisha kumeongeza wasindikaji wa mazao kufikia 40 kutoka wasindikaji 24 ambapo sasa wanafanya kazi kwa kushirikiana na wakulima zaidi ya 50,000.
Shughuli za kuwafundisha wasindikaji namna bora ya kufanya biashara kwa kuwapa ujuzi bora wakibiashara na namna ya kuangalia ubora wa mazao yanayoingia sokoni kumeinua sekta ya kilimo.
Pia wakulima wamehamasishwa kutengeneza kongani katika maeneo ya Majimoto,Itenja na MpandaHotel,Ambapo Kongoni hizo zinawafanya kurasimisha shughuri wanazozifanya kwenye upande wa masoko na kuwarahisishia kufanya biashara na wakulima kwa urahisi.
"..baraza la kilimo nchini imeweza kujenga maghara makubwa mawili pamoja na kukarabati magahara kumi na nane yenye uwezo kuhifadhi tani mia sita sitini katika kata ya Mishamo na Mnyagala wilayani Tanganyika" asema Lotti.
Ofsa Kilimo wa Halamashauri ya wilaya ya Mpimbwe Saad Nyagawa amesema kuwa uchumi wa wilaya hiyo unategemea kilimo cha mpunga,mahidi ,mtama na maharagwe ambapo hapo awali uzalishaji wao ulikuwa duni.
Moja ya mazao ya maharagwe Mkoani Katavi yakiwa yamelimwa kwa wingi |
Nyagawa amesema kupitia idara ya kilimo na mifungo kwa kushirikiana taasisi mbalimbali za utafiti za kilimo na mradi wa Tija Tazania wameweza kutoa elimu ya kilimo kwa wakulima inayozingatia matumizi ya mbegu bora pembejeo na uandaaji wa mashamba.
Ushirikiano huyo umekuwa chache kubwa ya maendeleo kwenye uzalishaji wa mazao
chakula ambapo kwa mwaka 2018/19 uzalishaji wa zao la mpunga ulikuwa tani
98,000 pekee hadi kufikia tani 123,000 kwa mwaka 2019/20.
" wakulima kwa moja moja wameongeza uzalishaji katika maeneo yako ya
kilimo ambapo wasitani wa sasa kwa uzalishaji kwa hekali moja ni gunia 15
hadi 18 hadi kufikia gunia 20 hadi 25 kwa ekali moja" amesema afsa kilimo
huyo.
Wakulima wamejifunza mbinu mbali mbali za uongezaji thamani wa mazao kupitia
mradi wa Tija Tanzania kwa kufundisha namna bora uzalishaji wa
mazao pamoja na hatua mbalimbali za uhifadhi mazao baada ya kuvunywa.
Ofisa Kiungo wa Miradi Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Peter Ntulo
amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa mazao kwenye sekta ya kilimo
kumechangia kwa kiasi kikubwa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na mazao ya
kilimo.
Ntulo amesema kuwa ukusanyajji wa mapato utokanao na tozo mbalimbali kwa
wakulima kumechangia halmashauri kuwa na fedha nyingi za utekelezaji wa miaradi
ya maendedeleo kwa wanananchi.
" sekta ya kilimo imekukuwa muhimu sana kwetu kutokana na faida
tunazozipata kutoka kwa wakulima...kwa maana hiyo kama halamashuri imedhamiria
kuendeleza kila juhudi zilizofanywa na Tija Tanzania kwa
masirfahi mapana ya taifa" amesema Ntulo.
Kwa upande wa baadhi ya wakulima Emmanuel Shigela mkazi wa kijiji cha Kikonko
amesema kuwa kupitia mradi wa Tija Tazania kumemtoa kwenye
umasikini licha ya kuwa mkulima kwa miaka mingi .
Shingela amesema kuwa kilimo duni kisicho zingatia utaalamu ndicho kilimo
ambacho kwa miaka mingi kimemfanya kuendesha kilimo amabacho wakati mwingine
hatutoshelezi mahitaji ya chakula kwenye familia yake.
Hivyo ameweka wazi elimu ya matumiz ya pembejeo pamoia na na mbegu bora
imemfanya kubadili maisha yake na kuwa ya juu huku akifanya maendeleo kwenye
familia yake kama vile kujenga nyumba ya kisasa pamoja na kuongeza mifungo
Amina Maulidi ambaye ni mkulima na mkazi wa kijiji cha Itenka A katika wilaya
ya Nsimbo amesema kuwa licha ya elimu waliyopatiwa ya kuzingatia kilimo bora
bali zana za kilimo za kisasa walizopatia zimetoa mchango mkubwa wa kuinua
uchumi wao.
Amina amesisitiza kuwa teknolija ya mashine za kilimo zimekuwa mwarobani wa
matumizi madogo ya nguvu huku kazi ikifanyika kwa weledi mkubwa.