Na
Mwandishi wetu KTPC,Mpanda.
HALMASHAURI
yoyote nchini itakayoshindwa kutekeleza agizo la
rais Dkt John Magufuli ifikapo januari 2021 ya kuondoa changamoto ya uhaba wa
vyumba vya madarasa pamoja na madawati kwa shule zote za sekondari,Wakurugenzi
na Wakuu wa Wilaya watawajibishwa bila huruma.
Agizo
la kuhakikisha kila Halamashuri inaondoa changamoto hizo limetolewa na Naibu
Waziri wa Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
OR-TAMISEMI,Davidi Silinde alipokuwa kwenye ziara ya ufuatiliaji wa fedha za
serikali zilizotolewa kwenye utekerezaji wa miradi mbalimbali katika Mkoa wa
Katavi.
Naibu
waziri huyo wakati akikagua vyumba vya madarasa vitatu vya shule ya Sekondari
Mwanganza Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi aliweka wazi kuwa suala la kila
mwaka wanafunzi kujiunga kidato cha kwanza kwenye shule za sekondari sio la
dharura kutokana kuwa ni kitu kinachofahamika.
“
sisi sote tunafahamu kuwa mwaka huu kunawatoto wako darasa la sita na mwaka 2022
ufaulu tunajua (pass rate) inafahamika kwa miaka mitano mfululizo inaeleweka
watoto wanafaulu kwa kiwango gani; kwahiyo hatuwezi kukaa kila wakati
tunajadili kila zinapofika nyakati kama hizi za miezi ya 11 na 12 ndipo
tunahagaika na madarasa hivyo ni lazima kuhakikisha ifikapo januari mwaka ujao
watoto wote wanakwenda shule” alisisitiza Silinde.
Vyumba
vya madarasa pamoja na madawati ni masula ambayo wakurugenzi na wakuu wa
wilaya wanapaswa kufahamu kuwa yanakwenda kwa pamoja kwani rais ameshatoa
maagizo kuwa kwa mwaka wa masomo utakao anza mwakani hakuna mtoto yeyote
anayepaswa kukaa chini awapo darasani.
“…natoa
rai kuwa hili agizo likamilike kwa wakati lakini vilevile halmashauri zote
nchini lazima ziwe na mpango mkakati endelevu ili mwakani ifikapo mwenzi wa 11
au 12 zisitokee changamoto kama hizi;Na hii ni kwa sababu pia tumezuia likizo
karibu zote za watumishi nchini hakuna kwenda rikizo hadi wakamilishe ujenzi wa
madarasa na utegenezaji wa madawat” alisema Naibu waziri huyo.
Awali
ya yote Naibu waziri huyo hajaridhishwa na kazi ya ujenzi wa vyumba vitatu vya
madarasa vya shule ya sekondari Mwangaza tangu serikali 26,Juni mwaka huu itoe
milioni sitini za ujenzi vya vyumba hivyo ambapo agetarajia kufikia sasa
viwe vimekamilika.
Kutokana
na uzembe uliofanywa na kusababisha kushindwa kukamilika kwa wakati madarasa
hayo Naibu waziri huyo alitoa ndani ya wiki mbili yawe yamekamilika madarasa
hayo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Michael Nzyungu akitoa
ufafanuzi wa kwanini wameshindwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa
alisema kuwa wamefanikiwa kupokea fedha hizo mwishoni mwa mwaka fedha 2019/20
ambapo zilikuwa zimefungwa na baada ya hapo zilianza kusoma 30,Octoba mwaka
huu.
Hivyo
Mkurugenzi huyo alimwahidi naibu waziri kuwa kutokana na kuwepo kwa vifaa vyote
vya ujenzi wa madarasa hayo atahakikisha ndani ya wiki hizo mbili wanakamilisha
ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa.
Naye
Mkuu wa Shule ya Shule ya sekondari ya Mwangaza Joseph Ntongolo alisema kuwa
licha ya uongozi wa shule kushukuru kupokea kiasi cha milioni sitini ujenzi
wa vyumba vitatu vya madarasa vilikabiliwa na changamoto ambazo ni vifaa
vya ujenzi katika manispaa Mpanda kuwa ghari sana ukilinganishwa na sehemu
zingine.
Aidha
ukosefu wa vifaa vya ujenzi katika Manispaa ya Mpanda hali imepelekea uagizaji
wa vifaa toka nje ya jambo linalochelewesha utekelezaji wa mradi kwa wakati.