Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera akiwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Mlele. |
Na
Mwandishi Wetu KTPC,Mlele.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Juma Homera ameagiza kukamatwa watumishi 12 wa umma na
wafanyabiashara watatu kwa kushindwa kurejesha zaidi ya milioni 34 ikiwa ni
thamani ya matofali ya theruji waliyojikopesha na kujengea nyumba zao.
Watumishi
hao wa halmashauri ya wilaya ya Mlele walijikopesha matofali 34,000 ya theruji
yaliyofyatuliwa kwa ajili ya ujenzi wa Hosptali ya wilaya hiyo inayojengwa
katika mji mdogo wa Inyonga.
Homera
alitoa agizo hilo hivi karibuni wakati wa ziara yake ya siku moja ya kikazi ya
kukagua ujenzi unaoendelea wa majengo saba ya hosptali ya wilaya ya Mlele.
Alibainisha
matofali 34,000 yaliyofyatuliwa chini ya kiwango hayakufaa kwa ajili ya ujenzi
wa hosptali hiyo na ndipo watumishi waliamua kujikopesha ili kujengea
nyumba ambazo wanaishi.
"...mmefyatua
matofali chini ya kiwango halafu zile tofali meshindwa kuzitumia kujengea
majengo ya hosptali ya wilaya ,watumishi mmejikopesha mmejengea nyumba zenu
ambazo sasa mnaishi" alisema Mkuu wa Mkoa huyo.
Baadhi ya watalamu mbalimbali na wananchi walio hudhuria kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homara Wilayani Mlele. |
Kutokana
na kutorudishwa fedha hizo kwa wakati Mkuu wa Mkoa huyo alimwagiza Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele,Alexius Kagunze ahakikishe
anasimamia kwa karibu ujenzi wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati.
"
inaonekana kwamba mlifyatua kwa makusudi tofali zilizo chini ya kiwango ili
muweze kujikopesha na kujenga nyumba zenu binafsi huku hosptali ikishindwa
kukamilika kwa muda muafaka" alisisitiza kwa ukali Homera
Naye
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mlele Alexius Kaguze alisema kuwa mradi
huo umegharimu zaidi ya biioni 1.8 zilizotolewa na serikali ambapo Halmashauri
hiyo ikitoa milioni 10 kutoka kwenye mapato yake ya ndani ili kukamilisha
ujenzi wa jengo la wazazi.
Kaguze
alisisitiza kuwa wanafanya kila jitihada ili kugakikisha majengo hayo yanakamilika
kwa muda muafaka huku akimwakikishia mkuu wa mkoa kuwa fedha hizo zinarejeshwa
haraka zaidi.
Kwa
upande wa wananchi wa Wilaya ya Mlele,Alphonce Zacharia licha ya kumshuru Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Juma Homera kwa hatua alizozichukua ili fedha zirejeshwe,Aliomba
watumishi wa umma kuwa wazalendo kwa taifa lao kwa kuwatumikia wananchi kwa
uaminifu.
Zacharia
alisema kuwa kama watumishi wa umma wanatakiwa kuwa waaminifu kiutendaji,ni
wazi kuwa hapataweza kutokea dosari kama ya kujikopesha matofali na kushindwa
kulipa kwa wakati.
Moja ya Jengo linalojengwa katika Hosptali ya wilaya ya Mlele likiendelea kujengwa |
Frola Anthony Mkazi wa mji mdogo wa Inyonga kwa upande wake alisikitishwa na kitendo cha watumiahi wa umma kujikopesha matofali na kushindwa kulipa fedha milion 34 ,huku akikazia kuwa kitendo hicho ni sawa na kuihujumu serikali.
"
ni jambo haliingii akilini, matofali yafyatuliwe chini ya kiwango wakati
wanafahamu kuwa ni ubora wa namna gani matofali ya ujenzi wa majengo ya
serikali yanapaswa kuwa...naomba rais Dkt Magufuli awachukulie hatua kali
watumishi wote waliohusika pamoja na waliojikopesha tofali hizo pia"
alisema Flora.