Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Mwandisi Godfrey Kasekenya (kwenye picha wa kwanza kutoka kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Muhando. |
Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi
Naibu
Waziri wa ujenzi na uchukuzi Mwandisi Godfery Kasekenya amesitushwa
na kasi ndogo ya ujenzi wa barabara kutoka Mpanda Mjini kwenda Inyonga yenye
urefu wa kilometa 105 inajengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya ujenzi ya
kichina inayoitwa China Railway Sevent Group
of China kwa thamani ya shilingi Bilioni 133.8.
Kasekenya
alishitushwana kasi hiyo hapo juzi wakati wa ziara yake Mkoani Katavi ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami kutoka
Mpanda hadi Tabora iligawangwa kwa wakandarasi watatu wa
kampuni za Kichina ambapo kampuni hiyo imepewa kujenga
barabara yenye urefu wa kilometa 105 kwa thamani ya Tshs
133,803,828,397.
Awali kabla ya kushitushwa na kasi hiyo ndogo ya ujenzi wa barabara hiyo inayotegemewa sana na wananchi wa Mikoa ya Katavi na Tabora pamoja na wafanya biasha wanaofasirisha mazao yao ya chakula kupeleka katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Mikoa ya Kanda ya Kati msimamizi mshauri wa mradi huo Mwandisi Peter Dondo alieleza kuwa mradi huo ulanza machi 2018 na unakiwa kukamilika Machi 21 mwaka huu.
Hata hivyo pamoja na kubakiza muda mfupi kutakiwa kuwa mradi huu umekamilika lakini hadi sasa mradi huu umetekelezwa kwa asilimia 55 tuu hari ambayo inaonyesha kuwa kwa muda uliobaki mradi huu hawezi kukamilka kama ambavyo mkataba unavyoelekeza
.
Mwandisi
mshauri alisema zipo sababu mbalimbali ambazo zimesababisha mkandarasi huyo wa
Kampuni ya Kichina kuwa nyuma ya mkataba wake huo ambao alitakiwa autekeleza
kwa muda wa miezi 36 sawa na miaka mitatu na sahizi kisha
tumia miezi 33 na kubakiza miezi mitatu tuu.
Alitaja
baadhi ya sababu zilizosababisha mradi huu kuwa nyuma ya mkataba
ni kampuni hiyo kuwa ni wabishi kupokea
ushaurikwani wamekuwa wakikaida ushauru ambao umekuwa ukitolewa na
msimamizi mshauri wa mradi huu na ndio maana wameshindwa hadi
sasa kuwa ndani ya mkataba wao .
Alitowa
mfano kuwa kuna kazi ambazo kampuni hiyo imekuwa ikishauri kuzifanya wakati wa
mvua lakini wamekuwa hawafanyi hivyo na matokeo yake kipindi hicho
kazi ambazo zilikuwa zinatakiwa kuendelea zimekuwa hazifanyiki
kutokana na ubishi wao
Meneja wamradi wa Kampuni ya China Raiway Seventh Group of China ( CRSG( Dong Hui alieleza kuwa wameisha omba waongezewe muda wa matengenezo hayo kwa kipindi cha miezi saba kwani hari ya jografia ya Mkoa wa Katavi kuanzia mwezi wa 11 hadi wa wanne mwishoni huwa ni kipindi cha mvua hivyo muda wao wa kufanya kazi huwa unakuwa ni mfupi.
Naibu
Waziri Mwandisi Godfrey Kasekenya alieleza kuwa haja
ridhishwa na kasi ya mkandasi huyo kwani muda aliyofanya kazi ni
mrefu kuliko muda uliobaki kwa hari hiyo mradi hauwezi kuwa umekamilika kama
ambavyo ulivyokusudiwa .
Hivyo
alimwagiza mkandasi mshauri kuandika barua kwake kupitia
kwa meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi juu ya sababu zilizosababisha kuchelewa
kwa mkandasi huyo katika ujenzi wa barabara hiyo na ndipo wizara itakapo towa
maelekezo kwa kampuni hiyo ya kichina