Na
George Mwigulu KTPC,Katavi.
Wizara ya
Maliasili na Utalii imeombwa kuondoa katazo la kuwazuia
Wakandarasi wanaotengeneza miundo mbinu ya barabara za
Mkoa wa Katavi kutoshimba vifusi vya udongo kwenye barabara
zinazopita ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi pindi wanapokuwa wanatengeneza
barabara.
Ombi
hilo limetolewa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Cremensia
Shayo wakati alipokuwa akisoma taarifa ya maendeleo na kazi
zinazofanyika katika Mkoa huu mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Mwadisi Godfrey Kasekenya kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi
hapo juzi .
Alisema
kuwa sheria za Wanyama pori zimekuwa ni kikwazo katika
shughuli za utengenezaji
Hivyo
aliomba Wizara ya Maliasili na Utalii⁰ kuiangalia upya sheria hiyo ili
matengenezo ya miundo mbinu yaweze kufanyika bila kuwa na kikwazo cha kuzuia
wakandarasi kuchimba kifusi na kukata miti pembezoni mwa barabara .
Shayo
alieleza kuwa zipo baadhi ya barabara zinazopita kwenye maeneo ya
Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambazo zinapita ndani ya Hifadhi a Taifa
lakini wakandarasi wanapokuwa wanataka kutengeneza miundo mbinu ya barabara
wamekuwa wakikatazwa kuchimba vifusi wala kukata mti na Tanapa.
Alizitaja
barabara ambazo zinapita ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi kuwa ni za
Sitalike kwenda Kibaoni yenye urefu wa kilometa 71,Maji Moto Inyonga
yenye urefu wa kilometa 130,na Barabara ya Sitaleke kwenda Kizi Mkoani Rukwa
yenye urefu wa zaidi ya kilometa 90.
Alishauri kuwa endapo kama sheria hii haitabadilishwa ni vema basi kazi
za matengenezo ya barabara kwenye eneo la Hifadhi ya Taifa ifanywe na
Tanapa wenyewe ili kuondoa usumbufu unaoendelea kutokea.
Naibu
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi Mwandisi Godfrey Kasekenya alisema kuwa swala
hilo ataliwasiisha katika Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuweza kulipatia
ufumbuzi zaidi .
Aliwapongeza Tanroads Mkoa wa Katavi kwa jitihada kubwa wanazofanya
katika utendaji wao wa kazi .
Kasekenya
alisema kuwa katikaIdara ambazo zipo chini ya Wizara hiyo Tamesa wamekuwa
hawafanyi viz
Hivyo Tamesa
inatakiwa muundo wake wa utendaji kazi uangaliwe upya ili waanze kufanya
kazi kwa ufanisi .