Na Mwandishi Wetu KTPC,Katavi
Wanajamii zaidi ya laki mbili
katika Mikoa ya Rukwa na Katavi wamepatiwa elimu juu ya utunza wa rasilimani za
kiikilojia zinazopatika katika maeneo yanayowazunguka ili rasilimali hizo
ziendelee kuwepo vizazi hadi vizazi.
Elimu hiyo iliyotolewa na Wanasheria
watetezi wa Mazingira kwa vitendo {LEAT} katika mradi wa Jumuiko la Pamoja
Suruhisho la Pamoja (JUPA SUPA) unaotekelezwa katika Mikoa hiyo miwili ya
Katavi na Rukwa imewataka wananchi wa Mikoa hiyo kutunza rasilimali
maji,misitu,Ardhi,Madini,wanyamapori na nyinginezo illi ziendelee kuwepo na
kutumika.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa
Mradi huo katika mkutano na wadau walioshiriki katika kutekeleza
Mradi,Msimamizi wa Mradi huo wa JUPASUPA Andrew Mariki aliwasihi sana wadau hao
kwenda kufanya kazi kwa kushirikiana na wanajamii waliopatiwa elimu hiyo
ya utunzaji wa rasilimali ili ziendelee kuwepo na kuwanufaisha katika maisha
yao ya kila siku.
"Lengo letu kubwa ni kutunza
rasilimali maji,Matumizi bora ya ardhi,upandaji wa miti ikiwemo urudishiaji wa
uoto wa asili,kutoa mawazo kwa mamlaka husika juu ya mbadala wa utumiaji wa
Zebaki kwa wachimbaji wadogo wa madini pamoja na utoaji wa msaada wa kisheria
pale unapohitajika"alisisitiza Mariki
Pia aliwataka wadau hao wa mradi
kuendeleza mabaraza ya ardhi,jumuiya za watumiaji maji,waangalizi wa rasilimali
pamoja na majukwa ya majadiliano kwani vyombo hivyo vipo kwa ajili ya usimamizi
wa rasilimali za vijiji.
Kwa upande wake Mwangalizi wa vyanzo
vya maji katika Kijji cha Matandalani Leonard Maembe ameupongeza Mradi wa
JUPASUPA katika kijiji chao umeleta mabadiliko makubwa kwani umebadili mila
kandamizi zilizokuwepo juu ya umiliki wa ardhi kwa wanawake,vyanzo vya maji
vilikuwa vikiharibiwa na mifugo lakini baada ya elimu ya utunzaji wa rasilimali
wamebadilika.
Nae mdau Elizabeth John wa kijiji
cha Ilemba alisema kuwa kupitia mradi wa JUPA SUPA ile dhana kandamizi ya
mwanamke kutotambulika na kupewa mamlaka ya kumiliki,kutumia na hata kuuza
ardhi imekwisha na kuomba mradi huo kama ikiwezekana uendelee tena kwa awamu ya
pili.
Mradi wa Jumuiko la Pamoja,Suluhisho
la Pamoja{JUPASUPA} unatekelezwa katika nchi 16 duniani na Tanzani ikiwa
mojawapo ambapo mradi huo umetekelezwa katika Mikoa ya Rukwa na Katavi ikiwa ni
mikoa ya kimkakati na kuwashirikisha wadau mbalimbali zikiwepo NGO'S za KAWODEO
NA UDESO zilizopo Mkoani Katavi.