Moja ya Jengo la Hosptali ya Wilaya ya Mlele likiwa limekamilika kwa ajili kutumika |
Na Ezrom Mahanga KTPC ,Mlele.
Wakazi wa Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wameanza kunufaika na huduma za afya katika Hosptali ya wilaya hiyo ambayo imeanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza.
Kuanza kutumika kwa hosptali hiyo ni miongoni mwa hosptali tatu za wilaya zilizojengwa Mkoani Katavi kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya,ambapo kwa muda mrefu wananchi walikuwa wakitumia umbali mrefu kusafiri kwa ajili ya kutafuta huduma za matibabu.
Baadhi ya wananchi wameeleza namna wanavyonufaika na huduma zinazotolewa hosptalini hapo na kueleza namna serikali ilivyopunguza mzingo wa kusafiri umbali kwenda kutafuta matibabu makubwa katika Hosptali teuli ya rufaa ya Mkoa wa Katavi iliyopo Manispaa ya Mpanda zaidi ya kilomenta mia moja.
Simon Warioba mkazi wa mji mdogo wa Inyonga anasema kuwa wilaya ya Mlele kuwa na Hosptali kubwa ni mwarobaini mwa kero ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikiwatesa ambazo ziliwafanya kujiona kama watu yatima waliotengwa na serikali kwenye kuletewa huduma muhimu ya kijamii kama hiyo ya hosptali.
Kutokana na kuanza kutumika kwa hosptali hiyo Warioba alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mlele kwa usimamizi bora wa ujenzi wa hosptali hiyo huku akimwomba kuzidi kuchapa kazi kwa masirahi ya Mlele na taifa kwa ujumla.