Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi Anna Lupembe. |
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi Anna Lupumbe ameendelea kuwa pamoja na wananchi wa jimbo lake kwa kuwahudumia hasa kwa kuhakikisha anatatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili.
Anna Lupumbe katika kutambua umuhimu wa watoto wote jimboni humo kuwa wanapata elimu bora hata kama wazazi wao wanaweza kuwa wanakabiliwa na changamoto za kiuchumi na kushindwa kukidhi gharama za masomo kama vile sare za shule,Lakini mbunge huyo ameweza kuzitatua kwa kutoa fedha ambazo zitasaidia kuondoa changamoto hiyo.
Kutokana na kitendo hicho kinachofanywa na mbunge huyo, Walimu,Wazazi na Walezi wamejitokeza na kusema kuwa chama cha mapinduzi kiendelee kutoa viongozi wazuri ambao watakuwa msaada kwa jamii.
Mwalimu wa shule ya MsingiMilambo Kata ya Litapunga Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Mwl Mshirimu. |
Halmashauri ya wialaya ya Nsimbo ni miongoni mwa halmashauri ndani ya Mkoa wa Katavi ambazo zinapambana na kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu katika mazingira mazuri kwa kujenga shule mpya za msingi na sekondari ambazo mwaka huu 2021.