Na Mwandishi Wetu KTPC,Katavi.
Maafisa liche wa halmashauri ya
Nsimbo,Tanganyika,Mpimbwe,Mlele,Manispaa ya Mpanda pamoja na afisa liche Mkoa
wa Katavi wameombwa kuwa sehemu huduma za Baba ,Mama na Mtoto ili kushiriki
vema kwenye utoaji wa elimu ya lishe.
Agizo hilo limetolewa jana na Naibu waziri wa afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt Godwin Mollel alipokuwa kwenye ziara ya siku
moja Mkoani Katavi kufuatia mkoa huo kuwa na watoto wengi wenye ugonjwa wa
utapiamulo licha ya mkoa kushika nafasi za juu kitaifa kwenye uzalishaji wa
mazao ya chakula.
Dkt Mollel alifafanua kuwa kama wizara haifurahishwi kuona
watoto wanakwenda hosptalini wakiwa tayari na ugonjwa wa utapiamulo bali idara
ya lishe inapaswa kutegeneza mpango mkakati wa kudhibiti ugonjwa huo kuazia
mtoto akiwa tumboni.
Maafsa Lishe wanapaswa kutambua ukubwa wa tatizo la lishe na
kama litapuuzwa kunauwezekano taifa likawa na watu waliohitimu kwa ngazi kubwa
ya elimu lakini bado wakawa na utindio wa ubongo kwa kushindwa kutatua
changamto za kimazingira na kuitumikia jamii kwa weledi na ufanisi mkubwa.
" Wakinamama wanapokuwa clinic hakikisha afisa Lishe
unakuwepo pale siku zote na ikiwezekana maafisa lishe wawepo kwenye mpango wa
malipo ya ziada na kuwa sehemu ya huduma ya mama na mtoto " alisema Dkt
Mollel
Naibu Waziri huyo alisema hakuna sababu ya kuona maafsa lishe
wanabaki maofisini bali wawepo kwenye huduma ya mama na mtoto kwa wakati wote
wakitoa semina zao ili kuepu watoto kuzaliwa wakiwa na uzito uliochini ili
waende majumbani mwao na tena warudishe hosptalini kutibiwa.
Vilevile Dkt Mollel alisema suala la lishe linahusu moja kwa
moja virutubishi vinavyopatikana kwenye vyakula,Hivyo yawezekana jamii
kuzalisha mazao ya chakula aina moja ya nafaka huku ikishindwa kuzalisha aina
nyingine ya mazao ya chakula,Kwa maana hiyo jamii pia inapaswa kupewa zaidi
elimu ya kilimo za mbogamboga pamoja umuhimu wake.
" kwa mfano kila mahali nilipokuwa nikitembelea mkoani
Songwe utaona mahidi pekee na wala huwezi kuona mbogamboga,hivyo yawezekana
watu wakawa na mahidi na wanakula ugali sana na hawana njaa bali hawali chakula
tofauti tofauti vya lishe" alisema naibu waziiri huyo.
Katika hatua nyingine Naibu waziri huyo aliweza kukagua ujenzi
unaoendelea wa Hosptali ya Mkoa wa Katavi,kukagua na kuzungumza na watumishi wa
afya wa hospatali teuli ya rufaa ya Mkoa huo huku akisiliza changamoto zake na
mafanikio yaliyopatikana pamoja na kukagua ujenzi uliokamilika wa hosptali ya
wilaya ya Tanganyika.
Katibu tawala wa Mkoa wa Katavi Abdallah Malela alisema kwa
kukili kuwa utafiti kupingwa kwa utafiti mwingine,Kwani tafiti zinazoonesha
mkoa wa Katavi kuwa na tatizo kubwa la ugonjwa wa utapiamulo huenda ni tafiti
za muda mrefu,Hivyo amekwisha kumwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt Omary
Sukari kuhakikisha kupitia ofisi yake inafanya zoezi la utafiti wa ugonjwa huo.
Malela alieleza kuwa kama serikali ya mkoa wanafanya juhudi zote
za kuutokomeza ugonjwa huo kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali wa afya ili
kuhakikisha watoto wa jamii ya mkoa wa Katavi ni salama na yenye afya njema.
Afisa Lishe Mkoa wa Katavi Asnath Mrema alisema kuwa hapo awali
elimu haikuwa imetolewa kwa kiwango kikubwa kwa jamii juu ya umuhimu wa lishe
bora ambayo inajumuisha namna ya uandaaji wa chakula jikoni na ulaji wake.
Hivyo kupitia mikakati ya mkoa ya kudhibiti ugonjwa wa
utapiamulo wanaendelea na utoaji wa elimu kwa kila mwananchi