RUWASA MPANDA YANUSURU NDOA ZA WANAWAKE

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Magamba Manispaa ya Mpanda wakipata huduma ya Maji baada ya Ruwasa Kuboresha Miundombinu hiyo.

 

Na Paul Mathias-Mpanda

Wananchi katika Kijjiji cha Magamba Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamenza kunufaika na huduma ya Maji kupitia Wakala wa huduma ya Maji safi na usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA kwa kuwaboreshea huduma ya upatikanaji wa huduma ya Maji kijijini hapo.

Baadhi ya Wananchi wa Magamba wakipata huduma ya Maji kijijini hapo

Wananchi katika Kijjiji cha Magamba Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamenza kunufaika na huduma ya Maji kupitia Wakala wa huduma ya Maji safi na usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA kwa kuwaboreshea huduma ya upatikanaji wa huduma ya Maji kijijini hapo

Wananchia hao wameeleza kuwa kuletwa kwa Huduma ya Maji kutoka Bomba la Kupampu kwa Mkono hadi kutumia mfumo wa umeme imepunguza adha ya upatikanaji wa huduma ya Maji ambapo awali walikuwa wanatumia muda Mrefu kupata huduma hiyo.

Amisa Rajabu Mkazi wa kijiji cha Magamba anasema ‘’wanawake tulikuwa hatulali usiku tunakuja kupampu Maji ila kwa sasa hivi maji tunateka vizuri bila shida yeyote kwa kutumia msukumo wa umeme ‘’amefafanua Amisa.

Amesema kuwa wakati mwingine ndoa zao zilikuwa zinatatizika kwa baadahi yao kwa kufokewa na waume zao kwa kuzani kuwa wapo katika mambo ya kusaliti ndoa zao kutokana na kutumia muda mwingi kusubiria maji kwa njia ya kupampu.

‘’Kwa sasa hivi sisi tulioolewa waumezetu walikuwa hawatuelewi wanasema tunakuja Bombani kwa mambo yetu kumbe ni changamoto ya maji ila kwa sasa hivi hakuna tatizo kabisa anasema’’ Amisa.

Kwa upande wake Kamtoni Changoma Mkazi wa Magamba ameiomba serikali kuongeza Magati kwa wingi katika Kijiji hicho ili kiweze kuendana na ongezeko la la watu waliopo kwa kutumia Gati moja.

‘’Hapa ndo kama ikulu kwa upatikanaji wa Maji bado vilevile hapatoshelezi tunaomba mtuongezee Magati hata Manne ili kidogo akina mama wachote maji hayo kwenye maeneo yao ‘’anasema Changoma.

Rehema Ramadhani anaeleza kuwa kulikuwa na shida ya Maji katika siku za nyuma na hapa anasema aaaa”Kiukweli sasa hivi maji tunayapata kwa raha siyo kama zamani tulivyo kuwa tunapampu mpaka tunachoka sasa hivi tunapata maji ya mserereko “

Amisa Rajabu Mkazi wa Kijiji cha Magamba akielezea namna Ruwasa Wilaya ya Mpanda ilivyoboresha huduma ya upatikanaji wa Maji kijijini hapo.

Dismas Mwandimu Msimamizi wa  chombo cha watoa huduma ya Maji ngazi ya Jamii Kata ya Magamba ameshukuru Ruwasa kwa Kuboresha Huduma ya Maji kijijini hapo kwa kuondoa adha ya akina mama kupampu kwa kutumia mikono lakini kwa sasa maji hayo kusukumwa kwa mfumo wa umeme.

‘’Tunaishuru serikali kupitia RUWASA kwa kuboresha Miundo mbinu ya Maji kutoka kupampu kwa mkono kuja mfumo wa kusukuma kwa umeme’’ anasema Mwandimu

Ameeleza kuwa katika siku za nyuma kulikuwa na mrundikano mkubwa wa watu waliokuwa wanasubiria kupampu Maji lakini kwa sasa hivi mfumo huo umepunguza msongamano kwa kuwafanya wananachi kuteka maji kwa kutumia muda mfupi na kuendelea na shughuli zao za maendeleo.

‘’Lile zoezi la kupampu kwa mkono lilikuwa linasabisha msongamano mkubwa walikuwa wanatoka usiku wa manane ila kwa sasa wananchi wanateka maji kwa wakati ‘’ amebainisha Mwandimu.

Ili kuhakisha wananchi wa Vijijni wanapata huduma ya Maji serikali imeunda taassisi ya Ruwasa inayoshughulikia upatikanaji wa maji kwa wananchi waishio Vijijini.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages