Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Tuungane,Marcel Kato (wa kwanza kutoka kushoto kwenye picha) akimkabidhi miche aina ya mikorosho Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Muhando. |
Na George Mwigulu KTPC ,Tanganyika.
Katika kuhakikisha uhifadhi wa mazingira na kuboresha afya za watu wa
Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi,Jamii imetakiwa kutumia
fursa ya kuwekeza kwenye kupanda miche aina ya mikorosho ili kuyanusuru
mazingira kwenye uharibifu pamoja na kuongeza vipato vyao.
Kwa kutambua umuhimu wa uhifadhi wa mazingira na afya za watu kuimarika
Tanzania Youth environmental network kwa ufadhili wa Shirika lisilo la
kiserikali la Tuugane walianzisha na kutekeleza mradi wa kuotesha miche ya
mikorosho na Sepulas wilayani humo.
Akikabidhi miche ya mikorosha zaidi ya 900,000 kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika
Saleh Muhando,Kaimu Mkurungezi wa shirika la Tuugane Marcel Kato alisema kuwa
wameamua kuotesha miche hiyo kwa ajili ya watu kulima zao la korosho na Sepulas
kwa kukuza uchumi na ustawi wa mazingira.
Kaimu Mkurugenzi huyo alieleza kuwa wamefanikiwa kuotesha zaidi ya miche
400,000 kitalu cha kijiji cha Mchakamchaka aina ya mikorosho katika
kata ya Mpandandogo pamoja na zaidi ya miche 100,000 kitalu cha Sibwesa
ikiwa ni mwendelezo wa miche 600,000 iliyogawiwa hapo awali.
Vilevile alifafanua wamefanikiwa kuotesha zaidi ya miche aina ya Sepulas
400,000 miti ambayo itapandwa katika ukanda nyanda za juu ya kijiji cha Mwese
ambayo mazingira yake yanaruhusu kustawi vema.
“Ninapenda kukiri kuwa kwa ushirikianio wa serikali ya
halmashauri,viongozi pamoja na wananchi tunaoupata wameonesha kuwa wako tayari
kwenye jitihada za upandaji wa miti ya mikorosho na Sepulas hivyo tutafikia
lengo la kuibadili zaidi Tanganyika kuwa ya kijani”alisema Kaimu Mkurugenzi
huyo.
Marcel alisisitiza wakulima wa wilaya ya Tanganyika wajitokeza kulima mazao
hayo kwani watakuwa na uwezo wa kujipatia kipato wakati huo wakihifadhi
mazingira kwa kuwa miti ni uhai.
Akipotea miti hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Saleh Muhando
alisema kuwa kwa kuzingatia malengo ambayo halmashauri imejiwekea pamoja na
wadau wa shirika la Tuugane ili kuhakikisha wananchi wanapata wanapata fursa
hiyo vema zoezi la ugawaji wa miche unafanyika bure bila malipo yoyote.
"ndugu wananchi miche hii niya bengu za kisasa inazaa kwa muda mfupi
ambapo ndani ya miaka mitatu inaanza kuzaa ikiwa miche hiyo inakubaliana na zao
la mahidi kwa kupanda miche ya mikorosho huku ukiendelea kulima zao la mahidi
hivyo wajitokeze kwa wingi kupanda miche hiyo " alisema mkuu wa wilaya
huyo.
Muhando alisema kuwa kwa sasa ni muda wa maafsa kilimo sio wa kukaa ofsini bali
waende kwenye mashaba ya wakulima kufanya kazi huku akiwataka kuadaa mpango
mahususi wa kuwakamata vijana wanaobaki kwenye vijiwe bila kujishughurisha na
kilimo.
Baadhi ya miche ya Mikorosho ikiwa katika kitalu ikiwa tayari kwa ajili ya kupandwa shambani. |
Aidha Halmashuri imejipaga kwenye mazao ya kimkakati ya ufuta,korosho kila
mwaka itaendelea kushirikiana na wadau pamoja na taasisi ya utafiti ili
kuendelea kupata mbegu bora za mikorosho,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo John Rumuli alishukuru sana shirika la
Tuugane kwa kuwapatia hapo awali miche 600,000 ya korosho na sasa zaidi ya
miche 900,000 ya korosho kwani wametimiza majukumu yao ipasavyo.
Rumuli aliongeza kuwa kipindi hiki cha mvua nyingi kunyesha ni msimo wa kupanda
miche hiyo ya mikorosho huku akiwasisitiza wananchi kutambua kuwa koroshpo ni
fedha kwani mahali ambapo korosho zimepandwa wameona ustawi maendeleo ukikua
kwa kasi.