Na Mwandishi Wetu KTPC,Nsimbo.
Wanafunzi wanao hitimu elimu ya
msingi katika halmashauri ya Nsimbo wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi
wanakabiliwa na changamoto ya kufanya vibaya kwenye mtihani wa mwisho wa taifa
kutokana na kupewa vitisho na kushinikizwa kufanya vibaya ili wasiendelee na
elimu ngazi ya sekondari.
Licha ya juhudi zinazofanywa na
halmashauri hiyo za kuhakikisha ujenzi wa shule hasa za sekondari unakamilika
ili kuondoa upungufu uliopo wa shule hizo na wanafunzi waweze kujinga na masomo
pindi wanapohitimu lakini wazazi/walezi hawajatambua umuhimu wa elimu.
Mohammed Ramadhani Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Nsimbo aliyasema hayo jana wakati akiongea na
waadishi wa habari ofisini kwake na kubainisha kuwa baadhi ya wazazi/walezi
wanawaambia watoto wao wafanye vibaya kwenye mitihani yao.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kwenye
mtihani wa mock mkoa uliofanyika octoba mwaka huu halmashauri yake
ilifaulisha kwa asilimia 99 kwahiyo walitegemea mtihani wa mwisho ufaulu
ugekuwa wa juu.
" tumefanya vizuri mtihani wa
majaribio lakini mtihani wa mwisho ufaulu umeshuka kwa asimilia 14 sawa na
ufaulu wa asilimia 85 " alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa matokeo hayo ya mtihani wa taifa
wamebaini kuwa kuna tatizo kwa baadhi ya shule na baadhi ya
wazazi/walenzi tumeshawabaini ambapo wanatarajia kuwaita kwenye
vikao na kuwachukulia hatua kali ili iwe mfano kwa watu wengine.
" kama kiongozi wa shughuri za
maendeleo tabia hizo nazikemea mara moja...kwa mfano shule moja yenye watoto
watatu wanafamilia moja ambapo walikuwa wanaogoza darasani ndio watoto pekee
waliofeli kwenye darasa lao ni kitu cha ajabu kwa sababu ni kitu ambacho
hatukikutegemea" alisrna Rammadhani.
Aidha alisema kuwa kufanya kwa
wazazi hao kitendo hicho ni kuzikatisha ndoto za watoto hao wakati watoto
wanauwezo.
Paulo Masanja mabaye ni mkazi wa
kijiji cha Urwila Halmashauri Nsimbo alikili kuwa kuna baadhi wa wazazi/walezi
kuwa na tambia za namna hiyo wakiwa na lengo la watoto wao wasiendelee na
masomo ya elimu ya juu kwa lengo la kuwa ozesha hasa kwa wasichana
Masanja alibainisha kuwa tabia hiyo
inarudisha maendeleo katika sekta ya elimu,hivyo kuiomba serikali
kuchukua hatua za kudhibiti.
Maria Alex mbaye ni mkazi wa kijiji
hicho aliiomba serikali kutunga sheria maalumu ya kuwadhibiti wazazi ambao wa
wanatabia ya kuwalazimisha watoto wao kufanya vibaya kwenye masomo yao.
Mzazi huyo alisisitiza kuwa endapo
sheria haitatungwa kuna uwezekano vitendo hivyo kuendelea daima na kudhoofisha
jitihada za serikali za kuwa na taifa la watu wenye elimu kubwa.