Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi,Christopher Nakua.
Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi.
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Mashitaka wanakusudia kuwafikisha Mahakamani Viongozi watatu wa zamani wa Mishamo Amcos Ltd kwa kosa la kutumia vibaya madaraka mabaya kichume na kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007.
Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa Katavi Cristopher Nakua amewataja viongozi hao wanaotarajiwa kufikishwa Mahakamani ni Pridance Anacredo Mark ambae mpaka wakati uchunguzi wa kosa hilo unapofanyika alikuwa ni Mwenyekiti wa Mishamo Amcos Ltd na Valantho Wiliam Gataro ambae wakati huo wa mwaka 2016 alikuwa ni Meneja wa Mishamo Amcos Ltd.
Nakua ameeleza kuwa viongozi hao wote wawili wakiwa kwenye majukumu yao utekelezaji kama viongozi walitumia vibaya madaraka yao kwa kuidhinisha mkopo wa fedha kiasi cha Tshs,4,000,000 kwa Freddy Moses ambae hakusitahili kupewa mkopo huu kwa kuwa hakuwa mwanachama wa Mishamo Amcos Ltd.
Watuhumiwa hao kwa kufanya hivyo walikiuka sheria na kanuni za ushirika na hata katika chama hicho zinazotaka mikopo ya fedha za chama sharti zitolewe kwa wanachama pekee.
Uchunguzi wa Takukuru ulibaini kuwa Freddy Moses mwaka 2014 kupitia Kampuni yake ya Mtuka Environmental Rehabilitation Compny ilisaini mkataba na Mishamo Amcos Ltd kwa ajiri ya kuotesha miche 484,924.
Amesema hivyo kwa kupitia ukaribu na watuhumiwa wakati wa kutekeleza mradi huu aliweza kukopeshwa kiasi cha fedha kinyume na utaratibu .
Amefafanua kuwa kwa mujibu wa kifungu kilichotajwa watuhumiwa hao walikiuka sheria katika utoaji wa mkopo na kusababisha Freddy Moses kujinufaisha na kupata manufaa ya faida asiyo kuwa anasitahili .
Nakua ameeleza kuwa kumekuwa na tuhuma nyingi zinazohusu vyama mbalimbali vya ushirika katika Mkoa wa Katavi na nchi kwa ujumla na tuhuma nyingi zimejikita zaidi kwenye matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha za vyama .
Hivyo Takukuru Mkoa wa Katavi wanaendelea kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo na uchunguzi ukikamilika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa .
Ametowa shukuru kwa wandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi kwa ushirikiano wao mkubwa katika mapambano dhidi ya Rushwa wanaoutowa kwa Taasisi hiyo