KWANINI WATAALAMU WA AFYA WANAWAOGOPA NGAMIA

 

Unaposogelea ngamia ukiwachukua vipimo unafaa kuwa muangalifu

Na Mwandishi Wetu KTPC

Inaaminiwa kuwa Covid-19 ilitoka kwa wanyama na kusambazwa kwa binadamuKwa sasa wataalamu wanatahadharisha kuwa kuna uwezekano kwamba huenda janga lingine linaloweza kulipuka kwa njia kama hiyo.

Kaskazini mwa Kenya, watafiti wanang'ang'ana kuzuia aina hatari ya virusi vya corona- Mers -kutoka kwa ngamia na kuingia kwa binadamu tena

75% ya magonjwa mapya yanayowakumba binadamu nyakati hizi yanatokana na wanyama kulingana na shirikisho la wataalamu wa magonjwa duniani linalodhaminiwa na serikali ya Marekani.

Wataalamu hao wamekwisha gundua na kushuhudia magonjwa mapya 1200 kutoka kwa wanyama. Wanadhania kuwa kuna magonjwa mengine 700,000 ya wagonjwa ambayo bado hayajafahamika.

Mnyama mmoja anayefugwa anayewatia hofu wataalamu hawa - ni ngamia.

Mnyama huyu wa jamii ya mamalia mwenye shingo ndefu hufugwa na mamilioni ya wakazi wengi wa Afrika Mashariki, Afrika ya Kaskazini , na maeneo ya Mashariki ya Kati.

Kwa wafugaji wake

Ngamia sio mifugo wa kawaida, kwani hutolewa harusini kama sehemu ya mahari, ni kitoweo na pia mali yenye thamini kubwa mtu anapokuwa nao.

Kulingana na wafugaji wa ngamia, mnyama huyu ni mnyama mwenye utulivu na amani. Lakini unapomsogelea ukiwa na sindano yenye dawa kutaka kumdunga au kifaa cha kumpima kuupitia pua lake, ndipo utakapojua hasira ya mnyama huyu .

"Anaweza kukupiga teke. kukutemea mate au hata kukukojolea ", anasema Millicent Minayo mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Washington, anayefuatilia maisha ya ngamia.

Minayo amekuwa akifanya uchunguzi kuwahusu Ngamia kwa muda wa miaka miwili, wafugaji wake, na wamiliki wake katika wilaya ya Marsabit Kaskazini Mashariki mwa Kenya . Anasema : "Mtu yeyote anayezikaribia anaweza kuambukizwa ".

Millicent Minayo na bagenzi be bambara ibyabugenewe bibakingira iyo bagiye gupima ingamiya n'abantu
Maelezo ya picha,

Millicent Minayo na wenzake huvalia mavazi maalum wanapowapima ngamia na watu

Ugonjwa huo wa ngamia unaofahamaika kama ' Middle East respiratory syndrome (Mers), aina mpya ya virusi vya corona umeonekana kuwa na makali ya kuua mara 10 zaidi ya Covid-19.

Ugonjwa huu ulipatikana Saudi Arabia mwaka 2012.

Hadi kufikia mwaka 2016, shirika la afya duniani (WHO) lilikuwa limeishapata sampuli zilizoonesha kuwa watu "1,761 waliugua Mers-CoV, na takriban 629 walikufa kutokana nao".

Baadae mwaka huo huo , ugonjwa huu ulisambaa katika hospitali na watu wakaambiwa kuwa maradhi haya yanaweza kumpata mtu yeyote yule na wala sio wafugaji wa ngamia peke yao wanaweza kuambukizwa.

Licha ya kwamba ngamia ndio wenye virusi hivyo, Mers ni tatizo kwa watu wote.

Kadri shughuli za watu zinavyoendelea kusababisha mabadiliko ya hali ya hewa na ukame mkubwa na wa muda mrefu, ndivyo wafugaji wanavyoacha ufugaji wa ng'ombe na mifugo mingine na kuanza ufugaji wa gamiakwani ndio wanyama pekee wanaoweza kuishi kwa wiki kadhaa bila kunywa maji.

Matokeo yake ni kwamba watu wengi wanaendelea kusogeleana na ngamia-jambo linalorahisisha zaidi kusambaa kwa maradhi hayo ya ngamia.

Minayo anasema "Tulileta utafiti huu nchini Kenya kwasababu kuna idadi kubwa ya ngamia, hususan katika wilaya hii ya Marsabit." Anasema yeye na watafiti wenzake walibaini virusi hivi mwaka 2019 katika ngamia 14.

Kwasasa wanajaribu kurusi hivi miongoni mwa watu wa Marsabit, ili kutafuta jinsi ya kukabiliana na kusambaa zaidi kwa ugonjwa huu kabla ya kusambaa kama Covid-19.

Nchi ya ngamia

Nchini Kenya kuna ngamia takriban milioni tatu, dadi hii ikiwa ni karibu 10% ya magari yote duniani, Kenya niya tatu baada ya Sudan na somalia kwa kuwa na idadi ya Somalia.

Serikali ya Kenya inasema kuwa Marsabit kuna takriban ngamia 224,000. Idadi hii ikiwa ni karibu sawa na idadi ya wakazi wa Marsabit.

Ufugaji huchangia 85% ya uchumi wa Marsabit, licha ya kwamba wakazi wa eneo hilo hufuga ng'ombe ngamia ndio uti wa mgongo wa uchumi wa eneo hilo, kutokana na kwamba ngamia ndio wanaoweza kuhimiri ukame katika eneo hilo.

Lakini kadri ngamia wanavyoendelea kuongezeka ndivyo hatari ya uwezekano wa kupata maambukizi kutoka kwao unavyoongezeka , kulingana na Dawn Zimmerman mtaalamu wa magonjwa ya wanyama katika taasisi ya Smithsonian Conservation Biology Iya uchunguzi wa magonjwa ya wanyama.

Anasema: "Magonjwa yapo kila mahali. Na endapo hatua hazitachukuliwa zinaweza kuwaambukia watu.

Kila asubuhi Millicent Minayo na Mwenzake Boru Dub Wato huenda kuwapima ngamia virusi vya Mers, huku wakiwa wamevalia mavazi maalumu ya kijikinga.

Huwaomba wafugaji kuwasaidia kuwakamata ngamia sitaili waweze kuwapima. Ngamia hawa ni wadogo kila mmoja hajatimiza umri wa miaka miwili.

Kubasha gupima ingamiya bisaba amayeri atandukanye n'abantu barenze umwe
Maelezo ya picha,

Kuwapima ngamia kunahitaji mbinu tofauti na itabidi zaidi ya mmoja

Dub Wato, ambaye amekulia katika maingira ya ufugaji wa ngamia katika Marsabit kutoka jamii ya Gabra anasema: "Ngamia ni mnyama mkubwa sana. Lazima uwe na nguvu ili kumkamata. Na sio nguvu anahitaji mbinu za ujanja kumkamata."

Mojawapo ya mbinu ni kumkata kwa kuanza na mkia wake huku ukiupapasa. Unapoweza kuukamata hawezi kwenda popote . "Mtu wa pili anaweza kushika sikio na mwingine mdomo ."

Ngamia hurukaruka na kujaribu kupiga mateke huku na kule au kuwapiga kwa magoti yake wanaojaribu kumkamata. Baada ya kuwakamata ngamia Dub Wato huchukua vipimo vyao kupitia puani , na kisha kuwachoma sindano chini ya masikio na kuvuta damu.

Baada ya upimaji wa ngamia, binadamu hufuata. Mmoja baada ya mwingine, Minayo huchukua vipimo vyao kupitia pua zao na kooni . Huku wakiongea na kufanya mzaha na kucheka, upimaji huendelea hivyo hivyo.

Siku yao ya kazi inapokamilika , Minayo na Dub Wato huvua mavazi yao ya kujikinga na maambukizi na kusafirisha sampuli za vipimo vyao kwa pikipiki hadi katika hospitali iliyopo mjini. katika hospitali huweka sampuli hizi katika friji zenye nyuzi joto 80 ili kuviwezesha kusafirishwa hadi mji mkuu Nairobi kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya virusi vya Mers.

Hata kabla ya kuibuka kwa mlipuko wa Covid-19, magonjwa 13 ya wanyama ikiwa ni pamoja na kifua kikuu(TB) homa ya ini, (hepatitis E ) na mafua ya ndege , yalikuwa yanasababisha maambukizi kwa watu bilioni na vifo vipatavyo milioni 2.2 kila mwaka duniani.

Iwapo virusi vya Mers vitaingia kwa binadamu vinaweza kusambaa kwa kasi kubwa.

nchini Saudi Arabia mwezi Disemba, 2019 na Januari 2020, watu 15 walipatikana na maambukizi ya Mers, watatu miongoni mwao walikuwa ni wahudumu wa hospitali.

"Kutokana na uwezo wa virusi vya aina corona wa kujibadilisha katika umbo jingine ina maanisha kuwa hakuna anayefahamu ni umbile gani la corona linaweza kumfikia binadamu " - Zimmerman.

Ndio maana ni muhimu sana kufanyika kwa utafiti wa magonjwa ya wanyamayanayoweza kusababisha majangakatika siku za usoni , anasema Zimmerman.

Ni wanyama wanaoliwa, maziwa yake ni kinywaji cha binadamu na binadamu huishi nao

Wafugaji wanaposafiri kutafuta malisho ya ngamia mbali na makwao, hulala na ngamia ili wawakinge na joto hususan nyakati za usiku kunapokua na baridi. Kunapokucha huwakamua maziwa na kuyanywa yakiwa mabichi-mara nyingine maziwa hayo huwa ndio kitu wanachokua nacho badala ya chakula kwa siku kadhaa au hata wiki nzima.

Ngamia anapofia jangwani wakati mwingine wafugaji hula nyama zao mbichi, kwasababu ya kukosa mahala pa kupika nyama yake.

Mienendo hii yote inaweza kusambazavirusi vya Mers.

Umwe mu barozi ari gupimwa iyi virus ya Mers muri Marsabit
Maelezo ya picha,

Mmoja wa wafugaji wa ngamia akipimwa virusi vya Mers katika wilaya ya Marsabit

"Tunawahamasisha kujikinga . Kuepuka kuwasogelea ngamia, na pale inapowezekana wavae barakoa na wanapowagusa wanawe mikono, kama tunavyofanya kujikinga na Covid-19'', anasema Dub Wato.

Lakini Ariko Lemilayon Lekonkoi , mkulima kutoka jamii Samburu anasema: "Kabla ya kuja kutuambia hatukua tunayafahamu hayo, hatukujua kuwa maziwa mabichi yanaweza kutusababishia ugonjwa. Lakini sasa tunafahamu, tunayapika kwanza ."

Lakini ngamia zinatia hofu kuliko wanyama wengine wanaofugwa na binadamu.

Ng'ombe wanaokamuliwa mara nyingi huchinjwa baada ya miaka karibu 6, mfano kama ng'ombe mwenye ugonjwa wa Brucellosis anakuwa na muda mfupi wa kusambaza bakteria hao kwa watu.

Mbuzi na kondoo huchinjwa baada ya miaka miwili. Lakini ngamia mwenye maambukizi ya virusi vya Mers au magonjwa mengine anaweza kumuambukiz binadamu katika kipindi cha 15 na 20 anayoweza kuishi dunia.

Lekonkoi anaufahamu ugonjwa wa Mers kwa jina bandia walilolpatia - Homa ya Ngamia (mafua ya ngamia ) -kwasababu Minayo na Dub Wato walimwambia kuuhusu.

Anafikiri amekwishaona ngamia wenye ugonjwa huo katika jamii yake : "Tunawaona ngamia wakikohoa-sawa na binadamu Turazibona zikorora - kimwe n'abantu. Ariko nyine twibanira nazo, ntabwo twazihunga".

Hali ndivyo ilivyo katika eneo muhimu la watu wanaozuia kueneo kwa virusi vya Mers

Wataalamu wa masuala ya kisayansi wanajaribu kuzuia majanga ya siku zijazo, wakiwapima watu na ngamia. Lakini dunia inabadilika sana inapokuja katika maambukizi ya magonjwa ambayo wanyama wanawaambukiza binadamu. Hata hivyo bado wataalamu wengi wanajiuliza iwapo mbinu za kupima magonjwa haya zinatosha au la.

Chanzo ni BBCswahili.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages