TANGANYIKA YATEKELEZA MIRADI YA ZAIDI YA BILIONI 18 KWA MIENZI SITA.

 



Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Dotto Kwigema(wa kwanza kulia)
Na George Mwigulu KTPC,Tanganyika.

Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi imefanikiwa kutekeleza miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni kumi na nane kwenye sekta mbalimbali ikiwa pamoja na ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo.

Utekelezaji huo wa miradi ni wa kipindi cha mienzi sita wa ilani ya uchanguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzi Julai 2020 hadi Januari 2021 katika wilaya ya Tanganyika ambapo jumla ya fedha Tshs 18,103,909,755.31 zimetumika ukilinganisha na bajeti nzima ya zaidi ya bilioni thelathini na tatu.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanganyika,Dotto Kwigema ambaye ni Afsa Mipango wa Halmashauri hiyo akisoma jana taarifa ya utekelezaji wa bajeti hiyo kwenye sherehe za maadhimisho ya kufikisha miaka 44 ya CCM katika viwanja vya shule ya sekondari Kasekese aliweka wazi kuwa mafanikio hayo kwa miezi sita yanatokana na juhudi kubwa inayofanywa kati ya serikali,chama na wananchi.

Dotto amefafanua kuwa jumla ya miradi 3,481 ambayo iko kwenye ujenzi wa nyumba za watumishi wa halmashauri ,ujenzi wa vyumba vya madarasa,ujenzi wa hosptali ya wilaya na ujenzi/ukarabati wa vituo vya afya na zahanati na miradi ya mikopo kwa vikundi (wanawake,vijana na wenye ulemavu)kupitia tengi la asilimia 10 ya mapato ya halmashauri.

Miradi mingine ni ujenzi/mategenezo ya barabara,ujenzi/ukarabati wa miradi ya maji na umeme vijijini yaani REA.

Kaim Mkurugenzi huyo amesema miradi iliyotekelezwa kisekta ni miradi ya utawala,elimu ya msingi/sekondari,afya,maendeleo ya jamii,kilimo umwagiliaji na ushirika,ufugaji nyuki,TASAF,Ardhi,Maliasili na mazingira,usimamizi wa barabara vijijini (TARURA),maji,bandari na ujezi wa kiwanda cha kuchambua pamba(NGS).

Akichambua baadhi ya miradi ya kisekta alibainisha kuwa kwenye afya miradi 29 yenye thamani ya 1,753,250,000/- imetekelezwa kwa kujenga wodi,vituo vya afya vitano,Hospttali ya Ikola.zahanati za vijiji tisa,ujenzi wa nyumba za watumishi viwili na ujenzi nyumba za msalani kumi.

Katika Idara ya maendeleo ya jamii sambamba na kutoa mikopo ya Tshs 266,183,300/- pia imewezesha wananchi kuinufaika na fursa za uchumi,kuwezesha uzalishaji,kuratibu na ufuatiliaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

“ tumefanya kazi kubwa ya kuratibu na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika masula mtambuka pamoja na kuelimisha jamii umuhimu wa miradui ya kitaifa kama vile ijenzi wa bandari Karema na kutumia fursa zilizopo kwa jamii” alisema Dotto.

Mohammed Mapengo,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tanganyika amesema kuwa kwenye maadhimisho ya miaka 44 ya CCM anakishukuru chama kwa niamba ya madiwani wote kwa kazi nzuri ya simamizi wa utekelezaji wa ilani ya chama ambayo imewafanya kushinda ushindi mkubwa kwenye uchanguzi mkuu Oktoba mwaka jana.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa taarifa iliyosomwa inaakisi juhudi kubwa inayofanywa na serikali ya wilaya kwani ndani ya miezi sita tu mambo makubwa yametekelezwa hivyo kuwaomba wananchini kuelendelea kutoa ushirikiano kwa serikali katika utekelezaji wa miradi kwa kuchangia fedha kwa hiali pale wanapoombwa kufanya hivyo.

Yasini Kiberiti ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanganyika kwa upande wake amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya mafundi ujenzi wa miradi mbalimbali kucheleweshewa malipo yao ya fedha.

Amesema kuwa vitendo hivyo vinarudisha nyuma juhudi za serikali za kuharakisha ujenzi wa miradi huku ikisababisha baadhi ya mafundi kujenga majengo ya umma chini ya kiwango kutokana na kufanya ubadhirifu wa kuiba baadhi ya vifaa vya ujenzi.

Vilevile licha ya kuipongeza halmashauri kwa kazi nzuri inayoifanya ameitaka kuhakikisha baadhi ya serikali za vijiji wilayani humo kuhakikisha kuwa na akauti maalumu benki ambazo zitatumika kuhifadhia fedha za maendeleo na kudhibiti ubadhirifu wa fedha za umma baaya ya kuonekana vijiji vingi hazina akauti za kibenki.



Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages