Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini,Sebastian Kapufi(wa pili kulia) akimpatia fedha Tasilimu 600,000/= kwa ajili ya kununulia bati ya kuenzekea nyumba yake iliyo ezuliwa na mvua kali ya upepo na mawe. |
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi amewapatia msaada wakazi wa Kata ya Ilembo ambao nyumba zao 62 zilienzuriwa na mvua iliyoambana na upepo mkali na kusababisha nyumba 62 kuenzuriwa na nyingine kuanguka hari ambayo imesababisha familia za watu 17 kukosa kabisa makazi ya kuishi akiwepo mzee wa (84)
Mvua hiyo ambayo iliyoleta maafa hayo ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika maeneo ya Mtaa wa Ilembo na Mapinduzi katika Kata ya Ilembo Manispaa ya Mpanda .
Hari hiyo imemlazimu Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi kufanya ziara kwenye eneo hilo na kuwapatia misaada wahanga hao kulingana na mahitaji yao ya haraka .
Miongoni mwa wakazi wa Kata hiyo Mzee Victoria mfinula (84) alisema kuwa toka nyumba yake ilipoenzuriwa na mvua hiyo iliyoambatana na upepo pamoja na mawe ya mvua amekuwa hana makazi ya kuishi .
Hivyo kwa sasa yeye na mke wake ambao wote ni wazee kutokana na umri wao kuwa mkubwa na kuwa na kipato kidogo hawana uwezo tena wa kurejesha paa la nyumba yao ambayo ilikuwa imeenzuka paa lake lote na ipo hatarini kuanguka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha .
Mbunge Kapufi kutokana na hali ambayo alikuwa nayo mzee huyo na familia yake alionekana kushitushwa na mazingira ya mzee huyo na ndipo alipowauliza wafundi waliokuwepo hapo gharama ya ujenzi wa paa la nyumba hiyo pamoja na bati unagharimu kiasi gani alijibu kuwa ni kiasi cha Tshs 600,000.
Baada ya kuambiwa kiasi hicho cha fedha alimkabidhi mzee huyo na kuagiza ujenzi wa paa ya nyumba hiyo ufanyike haraka sana hari hiyo ilimfanya mzee Victoria Mfinula alitowe shukurani kwa Kapufi na kutamka kuwa amemtowa kwenye shimo la kaburi kwani alijua kuwa nyumba yake haita pona tene .
Akilelezea hari ya tukio hilo Mkazi wa Mtaa wa Ilembo Evaristi Salinga alieleza kuwa mvua hiyo ilianza majira ya alfajiri huku ikiwa upepo mkali na radi za mara kwa mara na mvua ambayo ilikuwa inaangusha barafu kama mawe makubwa ambayo yamefanya uharibifu wa mazao na hasa mahindi .
Nae Jremia Bwilo alisema mvua hiyo ilianza saa kumi na mbili alfajiri na wakati akiwa ndani ya nyumba yake yeye na mke wake na watoto watatu wakiwa bado wamelala ambayo imeanguka aliona upepo mkali na mvua ya mawe na kisha aliona paa ya nyumba yake likienzuruliwa na kisha aliona ameangukiwa na matofali ya nyumba yake yaliomfanya apate majeraha kwenye mwili wake na bado anaendelea na matibabu .
Afisa Mtendaji wa Kata ya Ilembo Elimili Katendele alisema kuwa kwenye tukio hilo nyumba 62 zimeenzuliwa huku Kaya 17 zikiwa zimekosa makazi kabisa na wamehifadhiwa kwa majirani zao .
Alitaja sababu kubwa kwa kutokea kwa maafa hayo licha ya kuwa mvua ilikuwa ni kubwa iliyokuwa imeambatana na upepo ni wakazi wa eneo hilo kujenga nyumba zao bila kuwa na lenta .
Sababu nyingine ni eneo hilo kutokuwa na miti hari ambayo inafanya kuwa wazi na upepo kusambaa kwa urais .
Katentele alieleza kuwa kwenye ziara hiyo Mbunge huyo aliwatembelea wahanga wote 62 na aliweza kuwapatia kila mmoja fedha kadri ya mahitaji yao ingawa aliwaambia anajua wengine azitawatoleleza na wale walioumia aliweza kuwapatia fedha za matibabu fedha hizo ni zaidi ya milioni nane
Kwa upande wake Mbunge Kapufi alisema yeye mwenyewe ameweza kufika kwenye eneo hilo na kujionea kwa macho matatizo ya wananchi hao .