SIDO KATAVI CHACHU YA ONGEZEKO LA VIWANDA




Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Katavi Salome Mwasomola.

Na George Mwigulu KTPC,Katavi.

Viwanda 182 vimeanzishwa katika mkoa wa Katavi kutokana na serikali kupitia shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO),baada  ya kutoa elimu kwa wajasiriamali waliokuwa wakidhani  kujenga viwanda ni suala linalowahusu watu matajiri pekee.

Hayo yalibainishwa jana na Salome Mwasomola, kaimu Meneja wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo(SIDO) Mkoa wa Katavi alipoelezea namna ambavyo shirika hilo lilivyo wanufaisha wajasiriamali.



Moja ya Jengo la Wajasiriamali wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi linalotumika katika uzalishiaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na kuuzuia.

Ameleza  kabla ya kutoa elimu,wajasiriamali walikuwa wamekata tamaa ya kujenga viwanda kwa kushindwa kufahamu ni namna gani wanaweza kuanzisha,hasa kwa kupotoshwa na watu wasio nia njema kwao kuwa viwanda vinahitaji zaidi mamilioni fedha.

Salome amesema baada ya shirika kutoa mafunzo zaidi ya 18 ya aina mbalimbali kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa vikundi 63 yenye zaidi ya watu 317,watu wamehamasika kuanzisha viwanda ambavyo vinachangia ukuaji wa uchumi kwa kasi kwa serikali.



Hapa ni sehemu ya eneo la kukaushia chaki katika kiwanda cha Chaki Mkoa wa Katavi,ambapo meneja wa Mkoa wa SIDO ,Salome Mwasomola(wa pili kushoto) alipokuwa ametembelea kiwanda hicho.

"shirika limesaidia uanzishwaji wa viwanda kwa mfumo wa kongano ambapo jumla ya kongano mbili zimeanzishwa UWAVITE-Nsimbo na umoja wa wasindikaji nafaka Mpanda hotel manispaa ya mpanda" alieleza.

Kuanzishwaji wa viwanda hivyo vimetokana pia na shirika limewasaidia wajasiriamli kupata masoko kupitia maonesho ya sabasaba ,nanenane na SIDO kanda ambapo wajasiriamali 175 wameshiriki maonesho hayo ambayo yamewajengea uwezo na usubutu wa kuanzisha viwanda.

Kaimu Meneja huyo amesema licha ya mwitikio wa jamii kuchangia huduma zitolewazo na SIDO ni mdogo ikiwa na kugharamia mafunzo ili waweze kupata ujuzi zaidi wa kuanzisha viwanda,Ni changamoto ambayo kama shirika wataendelea kutoa elimu na kuhamasisha uanzishwaji viwanda kwa mfumo wa kongano.



Moja ya mashine ya kutengenezea Chaki katika kiwanda cha Katavi Chaki.

Aidha mkakati mwingine wa kukabiliana na changamoto kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ni kuendeleza ujenzi maalumu wa mtaa wa viwanda wa SIDO mkoa wa Katavi ambapo wajasirimali watatumia kama fursa ya kuanzisha viwanda mbalimbali.

Meneja masoko wa kiwanda cha Katavi Chalks,Tendi Katoro alisema bidhaa wanazozalisha zinakidhi ubora wa viwango vinavyotakiwa na shirika la ubora nchini (TBS) hiyo ikiwa ni kutokana na  ushirikiano mzuri kutoka SIDO Katavi.

Licha ya kuishukuru SIDO alisema kiwanda kinauwezo wa kuzalisha katoni 780 kwa mwenzi kiasi ambacho kinaifanya  kuwa moja ya viwanda kati ya 182 vinavyodharisha bidhaa kwa wingi zaidi.






Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages