HALMASHAURI YA NSIMBO YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA BILINION 16.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa aa Katavi,Hewala Malendeja(aliyesmama)


Na George Mwigulu KTPC,Katavi.

Baraza la Madiwa la Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa  Katavi linatarajia kukusanya na kutumia jumla ya zaidi ya Tshs Bilion 16.274 kwa mwaka wa fedha 2021/22  kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato,ambapo bajeti hiyo niongezeko la asilimia 0.25 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2020/21 ambayo ilikuwa ni zaidi ya bilioni 16.233

Mapendekezo hayo ya rasimu ya bajeti na  mpango wa maendeleo kwa mwaka 2021/22 wa fedha yalipitishwa hapo jana katika kikao cha baraza hilo liliofanyika  katika ukumbi wa halmashauri ya Nsimbo na kuongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri  hiyo Helawa Malendeja.

Akisoma mapendekezo hayo ya bajeti  Kaimu Afisa Mpingo wa Halimashauri ya Nsimbo Scholastica Njovu  alisema kuwa imependekeza  kukusanya  na kutumia  kiasi cha  Tshs 16,274,598,811.00 watakayo yapata kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani,fedha za ruzuku kutoka serikali na wafadhili mbalimbali.

Scholastica ameeleza kuwa kuongezeka kwa bajeti hiyo ni kutokana na uibuaji wa vyanzo vipya vya mapato ya vyanzo visivyolindwa (own sources proper) Tshs 1,000,980,000.00

Aidha amesema kuwa uandaji wa bajeti ya mwaka 2021/22 umezingatia muongozo wa bajeti iliyotolewa na serikali kupitia wizara ya fedha,maahitaji muhimu ya halmashauri ya Nsimbo kulingana na mpango makakati wa Halmashauri.

Kaimu huyo amesema pamoja ba kuandaa bajeti hiyo kwa kufuata vipaumbele vilivyopo,makisio yameathirika kutokana na viwango vidogo vya ukomo wa bajeti,Hivyo imefanya mambo mengine muhimu zaidi kutoweza kutengewa fedha au kutengewa fedha kidogo sana.

Alieleza kutokana na hali hiyo halmashauri imeomba serikali kuangalia upya uwezekano wa kutoa fedha kiasi cha Tshs 2,520,000,000.00 katika miradi ya maendeleo nje ya ukomo wa bajeti.

Mahitaji hayo maalum nje ya ukomo wa bajeti ni ujenzi wa vyumba 20 vya madarasa na nyumba za walimu 10 kwa ajili ya shule ya msingi na sekondari.

"..uhitaji mwingine ni ununuzi wa gari (Toyota land crusier VDJ 200R-GDMNZ) kwa ajili ya shughuli  za ofisi ya Mkurugenzi mtendaji" alisena Scholastica.

Aidha hitaji jingine ni ununuzi wa gari kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za wanyama wakali/waharibifu,Kwani zaidi ya asilimia 80 ya eneo la halmashauri ni hifadhi ya Taifa ya Katavi pamoja na ununuzi wa gari(lori) kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa Halamshauri ya wilaya Nsimbo Helawa Malendeja  aliwaomba madiwani wa Halmashauri hiyo kushiriki kikamilifu katika kubuni mbinu za kuongeza mapato ikiwa pamoja na kuhakikisha bajeti hiyo inaweza kutekelezeka kwa kushirikiana.

 Ameeleza kupitisha rasimu ya mapendekezo ya majeti ni kitu kingine na kukusanya mapato ni kitu kingine hivyo ni wajibu wa kila diwani kushiriki katika kuhakikisha mapato ya halmashuri ya Nsimbo yanaongezeka.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,Jamila Yusuph amesema suala la ukusanyaji kodi ni muhimu kwa halmashauri hiyo ili kuweza kutekeleza miradi ya maendeleo,Hivyo alisisitiza suala la kodi ya majengo kuwa inakusanywa kwa uhakika.

Jamila amesema kuwa kama halmashauri hiyo itajidhatiti kwenye ukusanyaji kodi itaweza kutekeleza kwa muda muafa miradi yake yote kwa masirahi ya wananchi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages