MBUNGE WA ZAMANI ATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE UHITAJI

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Katavi Dkt Pundenciana Kikwembe katika kutambua watoto wenye mahitaji ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya kuwasaidia watoto kwenye kituo cha kulea watoto cha Mtakatifu Yohane  wa II kilichopo Kata ya Nsemlwa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Msaada huo wa vitu mbalimbali amekabidhi kituoni hapo kwa Mkuu wa Kituo hicho Sister Rose Sungura wakati alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kuwatakia kheri na fanaka ya Mwaka Mpya wa 2026 kwa watoto hao wenye mahitaji.

Dkt Kikwembe amekabidhi kitanda kimoja,Godoro, Mafuta ya kula, Mchele,Sabuni na Vinywaji baridi ikiwa ni sehemu ya kuonyesha upendo kwa watoto hao kwa kuufikia mwaka mpya wa 2026.

Amesema watoto hao wanahitaji faraja kutoka kwa wazazi ,walezi na wadau mbalimbali nay eye kadri alivyojaliwa na mwenyezi Mungu ameona vema kutoa msaada huo.

Mlezi na Msimamizi wa Kituo hicho Sister Rose Sungura amemshukuru Mbunge huyo wa zamani Dkt Pundenciana Kikwembe kwa kutembelea kituo hicho cha kulelea watoto na kutoa mahitaji hayo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages