WANAFUNZI KUONDOKANA NA UHABA WA MADARASA ULANGA.

 



Na Mwandishi Wetu KTPC,Morogoro.

WANAFUNZI wa shule za msingi katika kijiji cha Namgezi tarafa ya Vigoi wilayani Ulanga wanatarajia kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 10 kufuata shule katika kijiji jirani cha Majanga baada ya kuanza kwa ujenzi wa shule kijijini hapo.

Uhamasishaji wa ujenzi wa shule hiyo umekuwa ukifanywa na Afisa Tarafa ya Vigoi, Shaban Kiduta lengo likiwa ni Wananchi kutumia nguvu kuanzisha ujenzi wake huku akidai kuwa kijiji hicho hakina shule ya msingi

Amesema kuwa, kijiji hicho ambacho kilianzishwa miaka 10 iliyopita kimekuwa likikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa shule ya msingi hali ambapo imechangia kiasi kikubwa watoto kupata huduma hiyo ya elimu. 

Amesema kukamilika kwa ujenzi huo utaongeza ufauli mkubwa kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakikutana na vishawishi mbalimbali pindi wanapoenda shule kutokana na kutembea umbali mrefu. 

Kiduta amesema hadi kufikia maamuzi ya kushirikiana na Wananchi kuanzisha mradi huo ni kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi ikiwemo, umbali mrefu wa kutembea kupata huduma ya Shule inayopelekea Utoro, mimba, na wanafunzi wa kiume kujiunga kwenye makundi mabaya.

Ameongeza kuwa mpaka sasa kupitia nguvu za Wananchi wamekamilisha ujenzi wa maboma ya vyumba vitano vya madarasa na Ofisi ya walimu katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo, ambapo ili Shule iweze kusajiliwa inahitaji Madarasa, Vyoo, nyumba ya walimu pamoja na Ofisi za waalimu. 

Mradi huo ulianza kutekelezwa mnamo Januari 2020 na hadi sasa una mwaka mmoja hadi kufikia hatua hiyo. Aidha Afisa Tarafa huyo ameshukuru ushirikiano mkubwa anaoupata kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri katika muendelezo wa Mradi huo. 

Ameomba wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada za Wananchi hao wa Kijiji cha Namgezi ili kutatua Changamoto hiyo ya Shule ya Msingi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages