SOKO LA MADINI KATAVI LAKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 3



Afisa Madini wa Mkoa wa Katavi,Jonas Mwano akizungumza na wanahabari namna sekta ya madini ilivyokusanya mapato.



Na George Mwigulu KTPC,Katavi.


Soko la Madini Mkoa wa Katavi limekusanya bilion 3.838 ikivuka malengo ya ukusanyaji mapato iliyopangiwa na serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21.


Soko la Madini Mkoa wa Katavi.


Soko la Madini Mkoa wa Katavi limekusanya bilion 3.838 ikivuka malengo ya ukusanyaji mapato iliyopangiwa na serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21.


Jonas Mwano,Afisa Madini wa Mkoa wa Katavi amesema hayo ofisini kwake alipokuwa alielezea jinsi ambavyo wamefanikiwa kuvuka malengo ya ukusanyaji mapato kutoka vyanzo mbalimbali.


Afsa Madini huyo ameweka wazi kuwa kulingana na makusanyo waliyopangiwa ya fedha bilioni 1.25 wamefanikiwa kuyavuka kwa asilimia 307.06 hadi kufikia Januari,31 Mwaka huu hiyo ikiwa ni kutokana na nguvu kubwa wanayoitumia kufikia malengo.


Alifafanua mchanganuo wa makusanyo hayo unatokana na Kodi ya madini Tshs 53,328,120/=,Ada ya kijiolojia Tshs 83,935,579/=,Mirabaha Tshs 3,031,565,675.76,Faini,adhabu na nyara Tshs 2,203,937.50 pamoja naUkaguzi na ada ya CL ni Tshs 667,217,144.97 ikifikia jumla ya Tshs 3,838,250,457.23 ya makusanyo yote.


Moja ya sehemu ya kuchoma madini ya dhahabu lililopo katika soko la madini


Takwimu za ukusanyaji wa mrabaha,ada ya ukaguzi na tozo ya huduma ya jamii kwa halmashauri zinatokana na mauzo ya madini tangu kuanzishwa kwa soko la madini Mei,2019 hadi Januari,2021.


Mwano amefafanua kuwa kwa sasa hakuna mauzo ya madini katika soko la Karema tangu kuanzishwa kwa soko hilo kwa sababu hakuna wanunuzi wa dhahabu kwa maana ya wafanyabiashara wenye leseni za biashara waliokwenda Karema.


"...hali hii ni kwa sababu hakuna wafanyabiashara walio kwenda Karema kutokana na meli iliyotarajiwa kutoka nchi jirani ya DRC Congo bado haijaanza kuingia katika Bandari ga Karema kupitia ziwa Tanganyika"alisema afisa madini huyo.


Aidha changamoto zingine ni mauzo ya madini kupungua kwa baadhi ya mienzi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambapo mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika Mkoa wa Katavi ambazo zimechangia uzalishaji na uchimbaji wa madini ya dhahabu kupugua.



Afisa masoko wa soko la madini Mkoa wa Katavi,Ndg Frank Malando alipokuwa akiwaelezea waadishi wa habari namna soko hilo limekuwa mkuombozi kwa wachimbaji wadogo.


Frank Malando,Afisa Masoko wa Soko la Madini Mkoa wa Katavi alisema kuwa tangu kuwepo kwa masoko ya madini yamesaidia kutambua kiasi cha madini yanayopatikana sambamba na kutambua aina mbalimbali ya madini yanayopatikana Mkoani Katavi.


Afisa Masoko huyo amesema kwa kuanzishwa kwa masoko hayo yamewasaidia wachimbaji wadogo wa madini kupata soko kwa urahisi ikiwa pamoja na utoroshwaji wa madini ambapo serikali ilikuwa ikipata hasara kwa kuhujumiwa mapato yake yanayotokana na mauzo ya madini.



Mhasibu wa wannuzi wa madini katika soko la madini mkoa wa Katavi,Ndg Mwaje Erasto


Mhasibu wa Makapuni ya kununua Madini kwenye soko la madini Mkoa wa Katavi,Mwaje Erasto ameiomba serikali kuhakikisha inajenga uzio katika soko la madini ili kuepusha wizi ambao umekuwa ukijitokeza kwa nyakati tofauti za watu wasio fahamika kuzoa mchanga kwenye maeneo ya kuchomea dhahabu.


Mwaje amesema kuwa kutoka na fedha nyingi serikali inazozikusanya kutoka kwenye sekta ya madini ni muhimu kuhakikisha miudombinu ya soko hilo wanaliboresha ili kukidhi mahitaji ya wanunuzi wa madini.



Moja ya jengo katika soko la madini Mkoa wa Katavi linalolalamikiwa na wanunuzi kutokana na kuwa limeharibika na kutishia usalama wa wafanyabiashara hao.





Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages