MAMA WA KAMBO AMUUA MTOTO KWA UJI WA MOTO

 

Na Mwandishi Wetu KTPC,MULEBA

Mtoto Arian Adelius mwenye umri wa miaka miwili amepoteza maisha baada ya kumwagiwa uji wa moto tumboni na mama wa kambo.

Mtoto Arian Adelius mwenye umri wa miaka miwili amepoteza maisha baada ya kumwagiwa uji wa moto tumboni na mama wa kambo.

Mtoto wa Kambo Arian amefikwa na mauti  baada ya kumwagiwa uji wa moto tumboni na mama wa kambo anayefahamika kwa jina la Leticia Protas mwenye umri wa miaka 42.

Inaelezwa kuwa mtoto huyo amemwagiwa uji wa moto  baada ya kuzuka ugomvi baina ya mama yake wa kambo  na  mama wa mtoto huyo Happiness Fidel wakati wa kikao kilichoitishwa na mume wao.

Imefahamika kuwa  lengo la kikao hicho kilicho itishwa na mume wao ni kumtambulisha mke mdogo kwa familia ili kuwa wamoja kwa kuishi kwa upendo.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema kuwa tukio hilo limetokea Machi 15 mwaka huu katika kijiji cha Kishanje Bukoba vijijini.

Kamanda huyo amefafanua kuwa wakati wa kikao kilichoitishwa na mume wa wanawake aliyetajwa kwa jina moja la Adelius mfanyabiashara wa Kyamyorwa wilayani Muleba ndipo tukio hilo lilifanyika.


Kamanda huyo amesema wakati wa kikao mke mdogo Leticia Protas aliyepelekwa kutambulishwa alikasirika na kunyanyua sufuria la uji kwa lengo la kummwangia mke mwenzake na kuwa baada ya mke mwenzake kukimbia alimmwagia mtoto na kumjeruhi vibaya tumboni, na hatimaye kusababisha kifo chake.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages