Baadhi ya Wananchi katika Kijiji cha Kakese wakipita kwenye Daraja hilo la watembea kwa Miguu linalounganisha Kata ya Kakese na Itenka. |
Na Paul Mathias-Mpanda
Wananchi katika kata ya Kakese Halmashauri ya Manisaapaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameishukuru serikali kwa kuwajengea Daraja la Watembea kwa Miguu linalopita Mto Mpanda na Kuunganisha Kata za Kakese na Itenka Wilaya ya Mpanda.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph [Kushoto akiwa na Moja ya Mwananchi wakivuka kwa pamoja kwenye Daraja hilo.
Wananchi katika kata ya Kakese Halmashauri ya Manisaapaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameishukuru serikali kwa kuwajengea Daraja la Watembea kwa Miguu linalopita Mto Mpanda na Kuunganisha Kata ya Kakese na Itenka Wilaya ya Mpanda.
Wananchi hao wamesema hayo mbele
ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph alipotembelea Daraja hilo kwa lengo
la kujionea namna Serikali ilivyojenga Daraja hilo kwa manufaa ya Wananchi hao.
Sophia Shija mkazi wa Kijiji cha
Kakese amaesema kuwa kipindi cha Nyuma kulikuwa na changamoto ya kuvuka kutoka
Kakese kwenda Itenka kutokana na mto huo kufurika maji na kukwamisha shughuli
za kiuchumi kwa wakazi wa Kata hizo.
Amebainisha kuwa kukamilika kwa
Daraja hilo litaimaimarisha shughuli za kiuchumi kwenye kata hizo Jirani.
Kwa upande wake Charles Madirisha
amesema kuwa mwanzoni kabla ya kujengwa kwa Daraja hilo walikuwa wanapita
kwenye Mabanzi watu walikuwa wanasobwa na Maji na kupoteza Maisha hasa wakati
wa Masika.
‘’Watu wengi sana wameenda na
Maji hapa tulikuwa tunapita kwenye Mabanzi kwahiyo tulikuwa tunateleza na mtu
anaenda na maji anasema Madirisha’’
Anabainisha kuwa kabla ya kujengwa kwa Daraja hilo walikuwa wanavuka kwa kuvushwa na watu kwa kutoa kiasi cha Shilingi Elfu Moja ila kwa sasa wana ishukuru serikali kwa ujenzi wa Kivuko hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila
Yusuph akiwa katika Daraja hilo amesema kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa kujenga
Daraja hilo pamoja na Kunyanyua barabara inayounganisha kata hizo kwa Gharama
ya Shilingi Milioni 162.
‘’Tunamshukuru sana Rais Dk Samia
Suluhu Hassan kwakutuletea fedha kwaajili ya ujenzi wa Daraja la hili la watembea kwa Miguu
pamoja na kunyanyua barabara hii ambayo tumeiona hapo fedha zilizotumika hapa
ni shilingi Milioni 262 ‘’anasema Jamila
Ameeleza kuwa eneo hilo lilikuwa
na adha kubwa kwa wanananchi kuvuka kutoka kata ya Kakese na Kata ya Itenka
hali ambayo iliwafanya wananchi kuchangishana wenyewe na kuweka Vivuko vya Miti
ambayo havikuwa na uiamara kwa wakati huo.
Saimon telephonesi mhandisi wa Tarura Wilaya ya Mpanda amesema pamoja na serikali kujenga Daraja hilo wao kama Tarura Wilaya ya Mpanda wameshaandika Barua kwa mtendaji mkuu wa Tarura kwaajili ya ujenzi wa Daraja la kudumu kwenye eneo hilo.