Katavi
Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anae shughulikia Sekta ya Ujenzi
Ludovick Nduhye amefanya ziara ya kutembelea barabara ya kutoka
Mpanda kwenda kwenye Bandari ya Karema ambayo inatarajiwa kuanza kujengwa
hivi karibuni mwaka huu kwa kiwango cha lami .
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anae shughulikia Sekta ya Ujenzi Ludovick Nduhye amefanya ziara ya kutembelea barabara ya kutoka Mpanda kwenda kwenye Bandari ya Karema ambayo inatarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni mwaka huu kwa kiwango cha lami .
Akizungumza wakati akiwa
kwenye Karema wakati wa ziara yake hiyo Nduhye amesemakuwa lengo la ziara
hiyo ni kuangalia barabara hiyo inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango mahali inapo
anzia na inapoishia .
Amebainisha kuwa lengo la
Serikali ya awamu ya sita imepanga kuboresha miundo mbinu
mbailimbali ya mawasiliano ya barabara katika kuhakikisha
inakuza uchumi wa nchi na kwa watanzania kwa ujula .
Amesema
ujenzi wa barabara hiyo ni muhimu kwa Nchi ya Tanzania na Nchi ya Kongo kwani
wanategemea mizigo ya kwenda kwenye Nchi ya Kongo itakuwa inasafirishwa
kwa barabara hiyo hadi kwenye bandari ya Karema kwa ajiri ya kusafirishia
mizigo na abiria wan chi hizi mbili .
Meneja wa Tanroads Mkoa
wa Katavi Mwandisi Martin Mwakabende ameeleza kuwa taratibu za
kuwapata wakandarasi watakao tengeneza barabara hiyo tayari umeisha anza kwa
kutangaza tenda ya kandarasi hiyo .
Amefafanua kuwa
zabuni za kuwapata wakandasi wa barabara hiyo utafanyika tarehe 30
ya mwezi huu wa tano ambapo ndio itakuwa siku ya kufunga
zabini zote za maombi na kuruhusu uchambuzi wa tenda
zitakazokuwa zimeombwa na makampuni mbalimbali ya ujenzi wa barabara ambapo ujenzi huo utachukua muda wa miezi 24..
Amesema kuwa barabara
hiyo imekuwa na changamoto kwenye baadhi ya maeneo hasa wakati wa kipindi
cha masika kwenye maeneo wanayolima mpunga bembeni mwa
barabara wananchi wamekuwa wakifungulia maji kwenye majaruba ya mpunga
na kuyaelekeza barabarani na kusababisha uharibifu wa barabara .
Nae Paroko wa
Kanisa Katoliki parokia ya Karema Padri Nikodems Kiyumana amesema
kuwa kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango cha lami kutaongeza furusa
kwa wananchi za kiuchumi kuanzia kwa mfanya biashara mdogo hadi mkubwa .
Pia kutafanya watu wawe
na usafiri wa uhakika wa kusafirisha mizigo yao hadi kwenye Bandari ya Karema
na kuisafirisha kwenda Nchi jirani ya Kongo na pia mizigo ya kutoka Kongo
itasafirishwa kwa urahisi hadi kwenda kwenye bandari ya Daress salaam kwa
kupitia barabara hiyo .
Padri Kiyumana ameeleza pia wageni wataongezeka hivyo itakuwa ni furusa kwa wafanya biashara wa nyumba za kulala wageni na pia tutapata furusa ya kujifunza mambo mbali mbali yakuleta maendeleo kutoka kwa wageni hao .