TAKUKURU KATAVI YABAINI MABATI YA ZAIDI MILIONI 220 YALIYONULIWA CHINI YA KIWANGO

Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Daud Lyamongo akitoa taarifa ya utendaji wa Takukuru kwa Kipindi cha Januari-Marchi

Na Walter Mguluchuma-Katavi

Taasisi ya  Kuzuia  na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Mkoa wa Katavi  imebaini  kukunuliwa  kwa mabati yenye thamani ya  zaidi ya shilingi  Milioni 220 yakiwa chini ya kiwango  yaliyonuliwa kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya  mpya ya sekondari  ya Kitaifa  ya Wavulana  ya Katavi.

Akitowa taarifa ya ufuatiliaji wa utelelezaji wa  miradi ya maendelo wa robo mwaka kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwaka huu kwa niamba ya Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi; Afisa TAKUKURU, Daud  Lyamongo  amesema  mabati hayo wameyabaini baada ya  ufatiliaji waliofanya  wa kukagua miradi katika sekta ya elimu.

Lyamongo   amebainisha kuwa  katika kipindi hicho  wameweza  kuokoa  kiasi cha  shilimgi  220,023,980 na wakiwezesha kupanda  kwa mapato ya stendi ya Mizengo Pinda  Manispaa ya Mpanda kutoka shilingi  500,000 kwa siku hadi  700,000.

Katika  utekelezaji  wa jukumu hilo waliweza  kukagua  utekelezaji  wa miradi  miwili  ya elimu  yenye  thamani ya  Bilioni 4.3 na waliweza  kubaini  uwepo  wa mapungufu  mbali mbali kwenye mradi wa shule  ya sekondari ya Wavulana Katavi.

Afisa hiyo wa TAKUKURU ameyataja mapungufu hayo kuwa ni  mabati yaliyokuwa yamenunuliwa kwa ajili ya   ujenzi  wa shule hiyo  yenye thamani ya  shilingi  220,023,980 wameyabaini yakiwa  chini ya kiwango .

Ametaja   kasoro nyingine kwenye ununuzi wa bati ambapo walibaini yako chini ya kiwango huku Mzabuni  alilipwa fedha  za   kununulia  mabati hayo  kabla hajayafikisha  kwenye   eneo  la  ujenzi  jambo ambalo n kinyume cha utaratibu  za manunuzi .

Baada ya  kubaini hayo  TAKUKURU Mkoa wa Katavi  walifanya kikao  kilichowahusisha  Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda, Mkuu wa Mkoa na Mzabuni  na kumtaka  mzabuni  abadilishe  mabati  na kuleta  mabati  yanayokubalika  kwa mujibu   wa muongozo wa Serikali .

TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi  na watakao kuwa wamebainika  kuhusiana na ununuzi wa bati hizo  pasipo kufuata utaratibu  watachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao .

Kuhusu uchambuzi wa mifumo  amesema wamefanya   uchambuzi  wa mfumo  wa ukusanyaji wa mapato  katika   stendi kuu ya Mizengo Pinda  Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda  na kuwezesha  kupandisha mapato  kutoka 500,000 hadi 700,000 ikiwa  ni ingezeko la shilingi 72,000,000 kwa mwaka .

Lyamongo amewakumbusha  wagombea  nafasi  mbalimbali  katika uchaguzi  mkuu wa 2025 kutojihusha  na vitendo vya rushwa  na kufuata  taratibu  kanuni  na  miongozo  iliyotolewa  na  tume huru  ya uchaguzi 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages