RC HOMERA: UZINDUZI WA KITABU  CHA MWONGOZO WA UWEKEZAJI NI LANGO KUU LA UKUAJI WA UCHUMI KWA MIKOA YA KUSINI MAGHARIBI.

 



Mkuu wa Mkoa wa Katavi,comrade Juma Homera akizungumza leo mapema na wanabari ofisi kwake juu ya uzinduzi wa kitabu cha mkoa kitakachofungua fursa za uwekezaji.
Na George Mwigulu KTPC,Katavi.

Katika kuhakikisha serikali ya mkoa wa Katavi unakuwa na nyenzo muhimu ya kujenga uchumi wake nakwa taifa  umejipanga kufanya uzinduzi wa kitabu kitakachoonesha fursa  za uwekezaji zilizopo mkoani hapo.

Juma Homera,Mkuu wa Mkoa wa Katavi amesema hayo ofisi kwake alipokuwa akiwaelezea wanahabari namna ambavyo mkoa utanufaika baada ya kitabu hicho kitakachozinduliwa.

Amebainisha kuwa uzinduzi wa kitabu hicho unatarajiwa kufanyika mnamo Mwenzi March,03,2021  ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania,Kassim Majaliwa(mb).

Mkuu wa mkoa huyo amefafanua kuwa kufuatia uzinduliwa  kwa kitabu hicho wawekezaji na wadau mbalimbali watapata fursa ya kuzitambua fursa zilizopo mkoa wa Katavi na kuwawezesha wawekezaji katika nyanja mbalimbali itakazokuwa ni lango kuu la uchumi kusini magharibi mwa nchi.



Waadishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi wakiwa katika majikumu yao wakati wakisikiliza maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Comrade Juma Homera.
Ameeleza kuwa kabla ya siku ya tukio serikali ya mkoa itafanya ziara ya kutembelea sehemu za uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwa pamoja na kutembelea hifadhi ya Taifa ya Katavi na mwambao wa ziwa Tanganyika ili kujionea vivutio na fursa za uwekezaji.

"...tukio la kutembelea vivutio litawafanya wawekezaji wa kutoka nje ya mkoa watapata fursa ya kukutana na wawekezaji wa ndani ili kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya kiuwekezaji"alisema Homera.

Mkuu wa mkoa huyo amefafanua kuwa kauli mbiu ya uzindunzi huo ni "Katavi Lango Kuu la Uchumi kusini Magharibi mwa Tanzania;Wekeza Katavi kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda",ambapo kauli mbiu hiyo inalenga kuhamasisha wadau kuwekeza katika Mkoa wa Katavi sambamba na kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania,DRC Congo,Burundi,Rwanda na Zambia.

Aidha kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya wameandaa zawadi kwa wawekezaji wa mwanzo watakaoonesha kujitokeza kuwekeza kwani mkoa una ardhi ambayo mazao yote yanastawi.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages