
Mkuu wa wilaya ya Mlele,Rechal Kasanda(wa pili mbele) akikagua baadhi ya miradi ya maendeleo.
Na Kibada Ernest AHHWM.
Mkuu wa wilaya ya Mlele Rechal Kasanda arejea ofisini baada ya kulazwa miezi saba kitandani akipatiwa matibabu kufuatia ajali aliyoipata akiwa katika majukumu ya kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe oktoba 2020.

Mwalimu Alexius Kaguze,Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mlele(mbele kushoto) akimwonesha mkuu wa wilaya hiyo Rechal Kasanda baadhi ya ujenzi wa miradi mbalimbali.
Mkuu huyo wa Wilaya Kassanda atembelea miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuanza kutembelea ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Mlele, Jengo la upasuaji Kituo cha Afya Inyonga “B,”Ukarabati mkubwa wa kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki,” Ujenzi wa Jengo la Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
Baada ya kutembelea miradi hiyo alikutana na watumishi kuzungumza nao,aliwapongeza watumishi wote kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo uchapakzi na ushirikiano walioutoa,kwa Viongozi waliokuwa wamekaimu nafasi yake wakati akiwa hayupo akiwa kwenye matibabu.
Pia alitoa pole kwa wananchi wote kwa kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Mhe Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli,sanjari na kutoa hongera kwa kumpata Rais Mpya Mhe Samia Suluhu Hassani tena mwanamke,kuwa Rais ambaye ndiye Kiongozi wetu kwa sasa, akaomba waendelea kutoa ushirikiano na kumwombea aweze kuongoza Taifa hili.
Mkuu huyo wa wilaya alieleza kwamba amerudi ofisini rasmi kuchapa kazi ili Wilaya ya Mlele iweze kusonga mbele kwa ushirikiano wa watumishi, waheshimiwa Madiwani, na Wananchi wote kwa ujumla wa Wilaya ya Mlele.
Aidha amesisitiza kusimimamia miradi yote ya maendeleo kwa ukaribu ili iweze kukamilika,pia amepongeza Halmashauri kwa kupata hati safi sanjali na kufanya vizuri katika suala la elimu hususani elimu ya Msingi kwa kuwa miongoni mwa Halmashauri zilizofanya vizuri Kitaifa na kuwa kati ya kumi bora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mwl Alexius Kagunze akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mlele mbele ya Mkuu wa wilaya ya Mlele Rechal Kasanda kama inavyoonekana hapo pichani,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mwl Alexius Kagunze akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mlele mbele ya Mkuu wa wilaya ya Mlele Rechal Kasanda kama inavyoonekana hapo pichani.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kikao cha watumishi kutoka Idara mbalimbali za Halmashauri na Taasisi zilizopo Wilayani humo katika kikao cha Mkuu wa Wilaya kilichofanyika ukumbi wa maktaba shule ya Sekondari Inyonga. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mwl Alexius Kagunze alieleza baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Mlele, Ukarabati mkubwa wa kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki, Umaliziaji wa jengo la upasuaji kituo cha Afya Inyonga “B,” Ujenzi wa Jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, na ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mwl Kagunze alitaja miradimingine kuwa ni Ukarabati/Ujenzi wa matundu 10 ya vyoo na mifumo ya maji kituo cha afya Inyonga B, Ukarabati/ujenzi wa matundu 5 ya vyoo na uwekaji wa mifumo ya maji kituo cha Afya Inyonga, Ukarabati/ujenzi wa matundu ya vyoo na uwekaji wa mifumo ya maji zahanati ya Ilunde.
Miradi mingine ni Ukarabati/ujenzi wa matundu 5 ya vyoo na uwekaji wa mifumo ya maji zahanati ya Nsenkwa, Ukarabati/ujenzi wa matundu 5 ya vyoo na uwekaji wa mifumo ya maji zahanati ya Mapili, Ukarabati/ujenzi wa matundu 5 ya vyoo zahanati ya kamsisi, Ukarabati/ujenzi wa matundu 5 ya vyoo na ujenzi wa mfumo wa uvunaji wa maji ya mvua zahanati ya Utende, na Ukarabati/ujenzi wa matundu 5 ya vyoo na ujenzi wa mfumo wa uvunaji wa maji ya mvua zahanati ya Ilela.

Mingine ni Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa Shule ya Sekondari Ilela, Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo shule ya sekondari Utende, na utengenezaji wa Madawati ambapo madawati 700 kwa Shule za Msingi yamekamilika na madawati 500 kwa shule za Sekondari yamekamilika.
Kuhusu suala la ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwa kipindi cha miaka mitano hajawahi kupata hati chafu,sanjali na kufanikisha katika suala la ukusanyaji wa mapato hadi kufikia machi walikuwa wamekusanya asilimia 94 mafanikio hayo ni kutokana na ushirikiano uliopo kati ya viongozi watumishi na wananchi kwa ujumla.