MAMBA,VIBOKO VYAZUA TAHARUKI NKASI.





Na  Walter  Mguluchuma KTPC,Nkasi.


DIWANI wa kata ya Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Ahsante Lubisha ameiomba wizara ya Maliasili na utalii kutoa haraka kibali ili halmashauri ya wilaya ya Nkasi ianze kuwavuna mamba na viboko katika kata yake kwani wamekuwa kero kiasi ambacho sasa wanaingia ndani ya nyumba za wakazi wa kata hiyo.

DIWANI wa kata ya Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Ahsante Lubisha ameiomba wizara ya Maliasili na utalii kutoa haraka kibali ili halmashauri ya wilaya ya Nkasi ianze kuwavuna mamba na viboko katika kata yake kwani wamekuwa kero kiasi ambacho sasa wanaingia ndani ya nyumba za wakazi wa kata hiyo.

Akizungumza na   mwandishi wa habari hizi  nje ya kikao cha Baraza la madiwani kilichofanyika mwishoni mwa wiki amesema kuwa wanyama aina ya viboko na mamba wamezaliana kwa wingi na kwakua serikali imefanikiwa kudhibiti ujanjiri hivi sasa wanyama aina ya viboko wamekuwa wengi wanazurula vijijini na wakikuta kuna nyumba ambayo mlango uko wazi wamekuwa wakiingia hadi ndani.

Amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa hali hiyo imezua hofu kwa wakazi wa vijiji vilivyopo katika kata hiyo huku wakazi hao wakishindwa kutoka kwenda kwenye shughuli zao za kiuchumi kwakua wanahofia maisha yao kutokana na ongezeko la wanyama hao hatari.

"katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita watu sita wameliwa na mamba akiwemo mwanafunzi Aidan Mwaloya(17) aliyeliwa na mamba hivi karibuni, alikua amechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na wengine kupata uremavu wa kudumu" amesema.

Naye kaimu Ofisa Maliasili wa wilaya ya Nkasi Frank Wakungwa amesema kuwa Idara hiyo imeandika barua wizarani kuomba kibali ili wawavune wanyama hao ambao wamekuwa wakizurula maeneo ya vijijini kwakua wanatoka ziwa Tanganyika huku wakifuata mito iliyojaa maji hadi vijijini na kuzua taharuki kwa wananchi.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi, Missana Kwangula amesema kuwa hivi sasa Kuna ongezeko kubwa la mamba na viboko katika kata kumi zilizopo mwambao wa ziwa Tanganyika na wamekuwa hatari kwa maisha ya binaadamu.

Amesema kuwa wanyama hao wamekuwa wakiharibu pia mazao ya wananchi Kama vile mpunga na tayari halmashauri hiyo imekwisha andika barua wizara ya Maliasili na utalii kuomba kibali ili iwavune wanyama hao ambao ni hatari kwa maisha ya wananchi.




Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages