
Na Walter Mguluchuma KTPC,Nkasi
KAYA zipatazo 320 katika Kata ya Kirando mwambao wa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi mkoani Rukwa zimebaki bila makazi baada ya kulazimika kuzikimbia nyumba zao kutokana na kuzimezingirwa na maji.

" Nyumba 320 ambazo ni za kisasa zimezingirwa na kujaa maji katika vijiji vya Mtakuja na Kichangani na kusababisha wananchi kuzikimbia nyumba zao" alisema.
" Kila upepo wa Kaskazi unapovuka ujazo wa maji ziwani unaongezeka na kusababisha mafuriko ambayo yanapeleka maji vijijini na nyumba za wakazi wa vijiji hivyo zinajaa maji pia" alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi,Missana Kwangula alisema tayari viwanja vya makazi vimetenga na kupimwa jirani na eneo la Shule ya Sekondari Nkasi ili vigawiwe kwa waathirika wa mafuriko ya maji ya Ziwa Tanganyika.
Alisema eneo hilo liko katika ukanda wa juu lakini changamoto iliyopo ni mwamko mdogo wa wananchi kuhamia na kujenga makazi yao kutokana na kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii.
Aliongeza kuwa pia ofisi ya Serikali na mwalo wa samaki umezingirwa na kujaa maji na hivyo kunachangamoto kubwa kwa wananchi hao kupata baadhi ya huduma.