TAKUKURU KATAVI WAPOKEA MALALAMIKO 80 YA RUSHWA KWA KIPINDI CHA MIEZI MITATU.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi,Christopher Nakua.


Na George Mwigulu,Mpanda

Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Katavi  kwa kipindi cha miezi mitatu ya kuanzia   Januari mwaka huu hadi Machi  wamepokea  malalamiko 80 kati ya hayo 26 yalihusu  vitendo vya Rushwa.

 Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Katavi  kwa kipindi cha miezi mitatu ya kuanzia   Januari mwaka huu hadi Machi  wamepokea  malalamiko 80 kati ya hayo 26 yalihusu  vitendo vya Rushwa .

 Hayo yamesemwa na Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa Katavi  Cristopher  Nakua  wakati alipokuwa taarifa kwa umma mbele ya wandishi wa Habari juu ya utendaji kazi  wa Taasisi hiyo  kwa Mkoa wa Katavi  kwa kipindi  cha  januari hadi  Machi  2021.

 Alisema  katika kipindi cha Januari hadi  hadi Machi  wamepokea jumla ya malalamiko 80 kati ya hayo  malalamiko  26 yalihusu  vitendo  vya Rushwa  na malalamiko 54 yalihusu makosa mengine .

 Katika kipindi hicho  majalada matatu  yalipelekwa  kwa DPP, kesi  mbili zilifunguliwa  Mahakamani  ambapo kwenye kipindi hicho  kesi moja  iliamuliwa Mahakamani  na watuhumiwa wote  katika kesi hiyo walitiwa hatiani   na kuhukumiwa vifungo au faini.

 Nakua alizitaja kesi hizo zilizofunguliwa Mahakamani  kesi ya kwanza ni CC.18/2021  ambapo Februari 10 mwaka huu Takukuru Mkoa wa Katavi walimfikisha Mahakamani  Pridance  Anacredo pamoja  Varanto  Gattaro ambao walikuwa  viongozi wa  Amcos  Mishamo  kwa kosa la  kutumia vibaya madaraka ya ofisi  kinyume na kifungu cha sheria cha 31.

 Aliitaja kesi ya pili  ni kesi  ni  kesi yenye Namba ECC.01/2021 ambapo  mnamo  tarehe 12 Februari  2021 walimfikisha Mahakamani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda   Juma  Mnyongalule  kwa kosa la kujipatia fedha kiasi  kiasi cha Tshs 3,750,000 isivyo  halali  kwa kuendelea  kulipwa  na kupokea  mshahara  kutoka shirika  la  Reli Tanzania  alikokuwa akifanya kazi hapo awali kama  fundi mchundo .

 Nakua alisema kwa upande  wa kuzuia na   ufuaatiliaji  wa miradi  ya maendeleo  wamefanya  kazi ya uchambuzi  wa mfumo  kuhusu   utoaji  wa vibali  vya ujenzi  nchini  katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda .

 Pia wamefanya kazi  ya ufatiliaji  wa fedha  za Miradi  ya Maendeleo  ambapo  miradi  kwa kufatilia miradi  inayohusiana  na mfuko wa Mandeleo  ya Jamii  awamu ya tatu TASAF  kwenye Wilaya ya Mpanda .

 Ufatiliaji huu wameufanya kwenye Kata za  Kawajense , Makanyagio ,Kazima , Nsemlwa  na Ilembo  uliokuwa na thamani ya Tsh.26,000,000 `` Alisema Nakua .


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages