
Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imefanikiwa kuokoa zaidi ya milioni 32 fedha hizo ni zile ambazo zilikuwa zichepushwe au kufanyiwa ubadilifu kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na 11 ya mwaka 2007.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imefanikiwa kuokoa zaidi ya milioni 32 fedha hizo ni zile ambazo zilikuwa zichepushwe au kufanyiwa ubadilifu kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na 11 ya mwaka 2007.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa Katavi Cristopher Nakua alipokuwa akitowa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari mwaka huu hadi mwezi machi mbele ya Wandishi wa Habari .
Alisema katika kipindi cha mwezi Januari hadi hadi Machi mwaka huu Takukuru Mkoa wa Katavi katika uchunguzi waliofanya kupitia operesheni mbalimbali walizofanya wameweza kufanikiwa kuokoa jumla ya Tsh,132,172,246 ambazo zilikuwa zichepushwe na kufanyiwa ubadilifu .
Nakua alibainisha kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha Tshs 250,000 zimeokolewa kutoka Mpate Saccos Tsh, 3233,000 zmeokolewa kutoka Manispaa ya Mpanda ambazo zimetokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani fedha hizo azikuwa zimetumika kama alivyokusudiwa kwa wa ajiri ya mkopo wa vijana ,wanawake na wenye ulemavu .
Fedha nyingine zilizookolewa ni fedha za ukusanyaji wa ushuru kwa njia ya kieletroniki (pos) tsh ,68,186,246. na kiasi cha Tsh 5,503,950 zimerejeshwa ikiwa ni malipo ya wakulima wa pamba ambazo zilikuwa kwenye kiwanda cha NGS.
Alifafanua kuwa fedha zilizorejeshwa kwa wananchi binafsi ni kiasi cha tsh milioni ,85.4 akiwemo mwalimu mstaafu Geoge Kanyukamamalunde aliyekuwa amedhurumiwa fedha mafao yake ya kustaafu .
Katika kipindi hicho katika kutekeleza jukumu lao la kuelimisha jamii na kuhakikisha umma katika mapambana dhifdi ya rushwa TAKUKURU Mkoa wa Katavi wametoa semina sita kwa makundi manne tofauti juu ya madhara ya rushwa na utendaji kazi wa TAKUKURU na onesho moja pamoja na makala nne.
Mkakati wa kipindi cha pili kutoka April hadi June wanatarajia kuongeza nguvu katika uchunguzi wa malalamiko yanayopokelewa hasa ubadhirifu wa fedha kwenye vyama vya ushirika.
Pia taarifa za ukaguzi wa mahesabu za halmashauri zote na pia kutoa elimu jwa wananchi pamoja na kushughurikia malalamiko mbalimbali ya wananachi yanyohusiana na rushwa kupitia TAKUKURU inayotembea.
Nakua alitowa shukrani kwa wanahabari kwa ushirikiano wao mkubwa katika mapambanon dhidi ya rushwa na anawaomba wandeleze mapambano hayo dhidi ya rushwa.