WAUMINI WA KIISLAMU MAJIMOTO WAMUOMBA MUFUTI KUTATUA MGOGORO



Na Mwandishi wetu KTPC,Mpimbwe.

Waumini wa dini ya Kislamu Kata ya Majimoto Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi wanaosali kwenye msikiti wa Almasjid Salamu  wamemuomba Mufti Mkuu Shekh Abubakar Zuber kutatua mgogoro uliodumu kwa miaka mitatu msikitini hapo. 
Waumini wa dini ya Kislamu Kata ya Majimoto Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi wanaosali kwenye msikiti wa Almasjid Salamu  wamemuomba Mufti Mkuu Shekh Abubakar Zuber kutatua mgogoro uliodumu kwa miaka mitatu msikitini hapo.

Mgogoro huo ambao umetokea tangu mwaka 2019  ni dhidi ya viongozi na waumini wa dini hiyo walioamuliwa na Balaza la Kislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Katavi kukabidhi na kuondoka kwenye msikiti huo kwa kile kinachotajwa kuwa sababu ya kuondolewa ni baada ya kusimikwa kwa mnara wa mtandao wa kampuni ya mawasiliano ya simu wa airtel ndani ya eneo la msikiti huo.

Akizungumza jana na wanahabari Katibu wa Msikiti wa Almasjid Salamu Kata ya Majimoto,Saidi Mustafa alisema kuwa  chanzo cha mgogoro huo unatokana na ofisi ya Bakwata Mkoa wa Katavi kuwaamuru  kukabidhi nyaraka za umiliki wa msikiti huo licha ya kuwa waliujenga kwa nguvu  zao na kwa msaada wa Taasisi ya Afrika Muslim Agent.

" ndugu wanahabari uwanja wa msikiti huu tulitafuta kwa fedha zetu na tukaujega bila ya bakwata kuchangia chochote kile  tangu mwaka 2015...Allah baadaye kashusha neema zake tukasaini mkataba na airtel wa malipo ya fedha 4,320,000/- kila mwaka  baada ya kuweka mnara huo" alisema.

Fedha za malipo hayo kutoka airtel walisema wamekuwa wakizitumia kwenye ujenzi wa madrasa na vyumba mbalimbali kwa ajili ya kupangisha  wafanyabiashara pamoja na fedha zingine kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu pale wanapofika msikitini hapo kuomba msaada. 
" ...tatizo liko pale wanapotufukuza sisi viongozi na waumini kwenye msikiti wetu,msikiti huu hauko chini ya bakwata hili liko wazi wazi kwa sababu kuna misikiiti mingi tu pia haiko chini ya bakwata.Na shida hii imeaza kutokea baada ya mnara huu wa airtel kuwekwa hapa kwani kabla ya mnara huu bakwata haijawahi kujitokeza" alisema Saidi.

Imamu wa Msikiti huo, Shekh Shaaban Juma alisema kuwa msikiti huo wameshirikiana waumini kuujenga chini ya Afrika Muslim Agent anashangazwa na viongozi hao wa mkoa Bakwata kuingilia kati msikiti wao hali ya kwamba wao sio wajenzi wa msikiti huo.

Shekh Shaabani alisema kuwa Afika Muslim Agent ndio waliojenga na kuwakabidhi nyaraka zote kuwa waaumini wa kisalamu wa Kata ya Majimoto ndio wamiliki wa msikiti huo na sio bakwata. 
''  kama imamu na kiongozi wa kiroho tunapata tabu sana kufikisha maneno ya Allah kwa sababu hivi leo athari inayoweza kutokea ni kubwa sana ,Nikijiangalia mwenyewe anaweza kuja mtu kutaka kuingia kwenye uislamu lakini akikuta migogoro mliyonayo anaweza kuwauliza kwamba je nikiingia kwenye uislamu niingie katika dini gani? hali ya kuwa Allah kwenye vitu hivyo tayari amesha tuelekeza" alisema Imamu.

Aidha alimwomba Muft  kuingilia kati mgogoro huo kwani kitedo hicho kinadhorotesha kazi ya ulezi wa kiroho maeneo hayo na kuzua sitofahamu ya waumini kutawanyika hovyo.


Hawa Selemani Mkazi wa Kata ya Majimoto alisema kuwa mgogoro huo umerudisha nyuma sana kidini kutokana na kuwa na marumbano makubwa ndani ya nje na baadhi ya waumini kufukuzwa.

Alieleza kuwa wamechoshwa sana na migogoro hiyo na kumwomba Mufti Mkuu wa Bakwata kuingilia kati ili kunusuru machafuko zaidi yanayoweza kujitokeza zaidi hapo baadaye.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages