Na Paul Mathias KTPC,Katavi.
Wafanyabiashara wa vyakula katika soko la Mpanda hotel Manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi wamelalamikia mwenendo wa kusuasua wa biashara katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wamebainisha hayo kwa nyakati tofauti mmoja wa wafanyabiashara Akizungumzia suala Hilo Schorastica Daniel amesema kwa kipindi hiki cha mwezi mtukufu kwa upande wa biashara ya nyanya pamoja na viazi Mbatata vinatoka taratibu tofauti na miaka mwingine katika kipindi kama hiki cha Mfungo wa Ramadhani.
Amesema kuwa tangu hapo awali kabla ya mwezi wa Ramadhani hali ya biashara ilikuwa siyo ya kulidhisha kutokana na hali ya hewa ya masika iliyopo.

Kwa upande wake mfanyabiashara katika soko Hilo Neema naftari amesema kuwa hali ya sasa hivi siyo ya kulizisha kutokakana na hali ya uchumi ya watu siyo ya kulizisha kutokana na kuwa bado bei ya mazao kama vile mahidi,maharagwe na Karanga walizovuna mashabani bei yake haijawa ya kuridhisha ili waweze kupata kipato kitakachowawezesha kununua mahitaji mengine ya kujikumu.
Ameongeza kuwa tenga la Nyanya wanalangua kwa kiasi cha shilingi Elfu 50 na utokaji wake umekuwa wa kusuasua kutokana na hali ya uchumi na changamoto za biashara kwa wakati huuu.
Nae mfanyabiashara Halima amesema kuwa sasa hivi mauzo yameshuka kutoka Tshs 150,000/= hadi Tshs 50,000/= au Tshs 30,000/= Kwa siku hali ambayo inawawia vigumu kufanya malejesho ya pesa katika taasisi za bank na wanachokifanya sasa hivi ni Kulinda mitaji yao ili waendeleee kufanya biashara katika hatua nyingne.
Ameeleza kuwa hatua hiyo ya biashara kwenda kwa mwendo wa kusuasua kwa wakati huu inatokana na hali iliyojitokeza katika kipindi hiki cha changamoto ya ugojwa wa Corona unaoiandama Dunia kwa sasa.
Kwa mara kadhaaaa katika kipindi cha mwezi wa Ramadhani imezoeleka kwa baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bidhaaa ya vyakula na mahitaji mengine yanayo endana na mfungo wa Ramadhani hali ambayo kwa Mkoa wa katavi bei ya vyakula imesalia kuwa ya kawaida kwa kwa wakati huu.