MABALOZI WA MITAA KUPITIA CCM MPANDA WATISHIA KUJIHUDHURU.


Na  Walter Mguluchuma KTPC,Mpanda.

Badhi ya Mabalozi wa CCM katika Kata ya Nsemlwa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi  wametishia kujiondoa katika nyadhifa zao za uongozi wa shina( BALOZI) kwa kile wanachodai kuwa wamekataliwa kuwa wanufaika wa Mpango wa kuzinusu Kaya masini Tasaf wakati wao hawapati ruzuku yoyote ya kutoka kwenye chama chao na hali ya maisha yao yako duni . 


Badhi ya Mabalozi wa CCM katika Kata ya Nsemlwa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi  wametishia kujiondoa katika nyadhifa zao za uongozi wa shina( BgALOZI)  kwa kile wanachodai kuwa wamekataliwa kuwa wanufaika wa Mpango wa kuzinusu Kaya masini Tasaf wakati wao hawapati ruzuku yoyote ya kutoka kwenye chama chao na hali ya maisha yao yako duni .

 Mabalozi hao wametowa kauli hiyo hapo  Mei 30 kwenye kikao cha kuwatambua walengwa wa Kaya maskini kilichofanyika katika Mtaa wa Migazini Kata ya Nsemlwa na kuleta mtaafaruku mkubwa kwenye mkutano huo

 MMoja wa viongozi hao  ambae ni Katibu wa Kata wa CCM wa Kata ya Nsemlwa  Charles Maganga alisema  kitendo cha kusomewa vigezo vya watu ambao wanatakiwa kujiunga kwenye mpango wa Tasaf  hauja wafurahisha mabalozi ambao wametishia kujiondoa kwenye nafasi hiyo baada ya kuambiwa kuwa wao hawana sifa za kuwa kwenye mpango wa Kaya maskini .

 Alisema kwenye mpango huu wamesomewa sharti ambalo linawaondoa viongozi wote wa vyama, dini na wale wa Serikali bila kuwa wameangalia hali zao za maisha wakati wao pia maisha yao yako duni sana kimaisha .

 Alitaja kigezo kingine walichotajiwa za watu ambao hawana sifa za kuwa kwenye mpango  ni  mtu ambae ana  mtoto ambae anaweza kumuudumia asisaidiwe kuwa mmoja wa wanufaika .

   Maganga alisema kuwa watu wanaohitajika kuwa kwenye mpango wameelezwa kuwa ni watu ambao hawana uwezo wa kula milo mitatu kwa siku,watu wenye ulemavu  na watu ambao ni maskini sana wa kipato ambao hata wakipata malazi wanakuwa hawana uwezo wa kununua panald alihoji kuwa watu kama hao ambao hawana uwezo wa kununua hata panald moja mbona hawapo wote walicha kufa .

 Amebainisha kuwa mabalozi hao wametishia kujiuzuru  nafasi ya ubalozi kwa kuwa wamekuwa wakifanya kazi kubwa wakati hawapati ruzuku yoyote ile hivyo ni jema wakajiondoa ili nawao wanufaike na Tasaf . 

 Mwenyekiti wa Mtaa wa Migazini  Ahamad  Kahena  alisema kuwa mpango ulikuwa unaenda vizuri  lakini kutokana na kitendo cha mabalozi  kutishia kujiuzuru  kumewafanya watu kwenye kikao cha kupendekeza majina watu washindwe kwa makusudi kutaja majina ya walengwa .

 Alisema  kuwa mabalozi wa ccm  hawana mishahara wanayo pata  na hata kwa viongozi wa ngazi ya tawi nao ni hivyo hivyo  hawapati chochote ndio maana wanataka kujiondoa ili nao wawe wanufaika wa Tasaf .

 Mwenyezaji wa Kaya maskini wa kutoka Manispaa ya Mpanda  Miliamu  Kavua  amesema mwitikio wa wananchi  kwenye mkutano wa kupendekeza majina ya walengwa umekuwa ni mdogo baada ya mabalozi wa nyumba kumi kutotowa ushiriiano wa kutosha .

 Amesema viongozi hao wamekuwa wakilalamika kuwa vigezo  vimewaondoa  wakati wao  hawapati kitu chochote  kwenye chama chao .

 Hivi karibuni viongozi wa Kata mbalimbali wakiwemo na madiwani walipatiwa mafunzo ya uwelewa  wa pamoja juu ya mpango wa  Tasaf  ili wawezekuwaelisha wananchi waondokane na  changamoto ya kutoelewa mpango huu kama awamu iliyopita













Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages